Di Maria akishangilia bao lake wakati Argentina ikikubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Ufaransa.
Kylian Mbappe akiifungia Ufaransa bao katika mechi dhidi ya Argentina.
Kylian Mbappe wa Ufaransa akichezewa vibaya na Marcos Rojo wa Argentina na kuzalisha mkwaju wa penalti.
Kylian Mbappe wa Ufaransa, akiwa katikati ya msitu uliojumuisha wachezaji wenzake na wale wa timu pinzani ya Argentina. Hapa alikuwa akifumua shuti kuifungia moja kati ya mabao yake.
Mercado wa Argentina akiwa amembeba Messi wakishangilia bao lake wakati wa pambano la 16 Bora dhidi ya Ufaransa. Hata hivyo Ufaransa ilichapwa mabao 4-3.
Mshambuliaji wa Argentina, Angel de Maria, akijipinda kufumua shuti kuiandikia timu yake moja kati ya mabao matatu katika kipigo cha 4-3 walichopata toka kwa Ufaransa.
N'Golo Kante akimiliki mpira huku akizongwa na Messi.
Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, akifunika uso wake kutoamini namna kikosi chake kilivyokuwa kikidhalilika wakati wa pambano la 16 Bora Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.
Nguli wa Argentina, Diego Maradona, akishangilia moja ya mabao ya timu yake ilipokuwa ikiumana na Ufaransa.
Ufaransa yaua.
Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia moja ya mabao yao katika mechi dhidi ya Argentina
MOSCOW, RUSSIA
HAKIKA Wamepata Tabu Sana. Ndivyo unavyoweza kuelezea hali waliyokumbana nayo leo Argentina katika pambano la 16 Bora ya Fainali za Kombe la Dunia (Fifa World Cup 2018), baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Ufaransa.
HAKIKA Wamepata Tabu Sana. Ndivyo unavyoweza kuelezea hali waliyokumbana nayo leo Argentina katika pambano la 16 Bora ya Fainali za Kombe la Dunia (Fifa World Cup 2018), baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Ufaransa.
Hilo lilikuwa pambano la kwanza 16 Bora, lililopigwa kwenye Uwanja wa Kazan Arena mjini Kazan, nchini Russia, zinakoendelea fainali hizo za 21, zinazofikia ukomo Julai 15 kwa fainali ya michuano hiyo kurindimishwa jijini Moscow.
Ufaransa walitinga hatua hiyo na kukutana uso kwa uso na Argentina baada ya kumaliza kinara wa Kundi C, huku miamba hao wa soka la Amerika Kusini wakimliza nafasi ya pili katika Kundi D la fainali hizo zisizo na bingwa mtetezi baada ya Ujerumani kung’olewa.
Ikicheza soka la kuelewana na kushambulia kwa kasi, Ufaransa ilitangulia kupata bao la penalti dakika ya 13, lililowekwa kimiani na Antoine Griezmann, ambalo lilidumu hadi dakika nne tu kabla ya mapumziko, Argentina iliposawazisha kupitia Angel di Maria.
Kipindi cha pili, Argentina walikuja vizuri zaidi na kufanikiwa kupata bao la uongozi lililowekwa kimiani na Gabriel Mercado, kabla ya Ufaransa kutuliza akili nao kufanikiwa ‘kuchomoa’ mnamo dakika ya 57 kutpitia bao la Benjamin Pavard.
Baada ya hapo, Ufaransa walikuwa wazuri zaidi kwa kubadili upepo na kufunga mabao mawili kupitia yoso wao Kylian Mbappe, aliyefunga mara mbili ndani ya dakika nne (dakika ya 64 na 68), kabla ya Argentina kupata bao la tatu dakika ya 90 kupitia mtokea benchi Sergio Aguero.
No comments:
Post a Comment