HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2018

SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUTOKA NSSF

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizunguza wakati wa Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kwa Wajasiliamali ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaingiza wote walio kwenye sekta isiyo rasmi katika Mifuko ya Jamaa.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwemo wawakilishi wa Benki za Azania na NMB.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibisha Sera wa Shirika la Mifuko ya Jamii (NSSF), Mariam Muhaji akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo.
Baadhi ya Viongozi wa NSSF walioshiriki pia katika Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mkoani Kilimanjaro.
Muwakilishi wa Benki ya NMB Tawi la Nelson Mandela Moses Koda akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.
Muwakilishi wa Benki ya NMB ,Adeline Gabriel akichangia jambo wakati wa Mafnzo hayo.
Mgeni rasmi ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo yanayoendelea maeneo mbalimbali nchi nzima.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini

SHIRIKA la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na Benki za Azania,NMB na NBC kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanachama wake watakao ingia kwenye mpango wa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, lengo likiwa ni kupunguza hali ya umaskini.

NSSF imeanza utekelezaji wa mpango huu baada ya maboresho ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyotoa majukumu kwa shirika hilo kuboresha na kushuhulikia sekta isiyo rasmi ambayo inatajwa kuwa kwa muda mrefu imetelekezwa.

Katika kuhakikisha elimu hii ya inawafikia wananchi wengi ,NSSF imeanza kufanya mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali ili kutoa hamasa na baadae kuwaingiza katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wananchi wote ambao wako kwenye sekta isyo rasmi..

Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Moshi,Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Kippi Warioba akatumia nafasi hiyo kutoa rai kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya ubadhirifu.

Kwa upande wao washiriki wa Semina hiyo wakiwemo viongozi wa Benki zilizoingia mkataba na NSSF katika kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanachama walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo wameelezea matumani yao juu ya mpango huo wa NSSF.

Wanachama ambao watanufaika na mpango huu ni wale watakao toka kwenye vikundi vyenye sifa za mikopo ambayo itasimamiwa na Benki ya Azania zikiwemo Saccos na Amcos zaidi ya 100.

No comments:

Post a Comment

Pages