Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akihutubia kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Nchi 12 za Afrika uliofanyika wiki iliyopita nchini Kenya,
Baadhi ya washiriki kutoka Tanzia wakiwa kwenye mkutano huo. Watatu kutoka kushoto ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.
Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga (kulia) na Katibu wa Stellah Joel wakipata chakula wakati wa mkutano huo.
Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akiwa mbele ya moja ya majengo marefu nchini Kenya.
VIONGOZI wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) wameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nchi 12 za Afrika uliofanyika Nairobi nchini Kenya.
Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kuona fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia wanamuziki katika nchi zao na jinsi ya kuzitatua changomoto.
Akizungumzia mkutano huo, Rais wa TAMUFO, Dk. Kisanga alisema wameshiriki mkutano huo kwa ajili ya kutafuta fursa za kimataifa ili kuinua muziki wa Tanzania na pia kuelezea jinsi gani mwanamuziki anaweza kulikomboa Bara la Afrika kiuchumi na katika masuala ya kijamii.
"Kushiriki katika mkutano huu kwetu sisi ni fursa kubwa hivyo tuna kila sababu ya kujivunia kwani tumejifunza mambo mengi" alisema Dk.Kisanga.
Kisanga alitaja nchi zilizoshiriki mkutano huo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Swaziland, Ethiopia, Ruanda, Madagascar, Nigeria, Malawi na Botswana.
No comments:
Post a Comment