HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2018

ASLEY, SHILOLE KUNOGESHA KAMPENI YA RUDI NYUMBANI KUMENOGA

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania, TTCL leo limetiliana saini na wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley watakaoshiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
 
Akizungumza na Waandhishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino Mhandisi Isaack Kamwelwe Agosti 31 mwaka huu Mkoani Katavi.
 
Amesema lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikishia taarifa wananchi kuhusu TTCL mpya ambayo kwa sasa imefanya mabadiliko makubwa katika biashara ya Huduma za Mawasiliano hapa Nchini.
 
Asema Tamasha hilo ambalo halitakuwa na kiingilio litakuwa la aina yake ambapo wasanii wamejipanga kutoa burudani kabambe huku wananchi wakipata fursa ya kuelimishwa kuhusu Shirika la TTCL, Huduma zake na majukumu yake ya msingi pamoja na kujipatia Sim Kadi na kujisajili bure na kuuziwa bidhaa mbalimbali za TTCL kwa bei nafuu.
 
“Hii ni kampeni ya Mkoa kwa mkoa, ambayo pia itatumika kutatua changamoto na kero mbalimbali walizonazo wateja wetu juu ya huduma na bidhaa zetu” alisema Kindamba
 
Kwa upande wake Zuena Mohamedi kw aniaba ya msanii mwenzake amesema amejipanga kutoa burudani kabambe itakayotoa hamasa kwa wananchi kupenda vya kwao na hivyo kurudi nyumbani kwa kutumia Mtandao wa TTCL.
 
“Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe wazalendo tutumie bidhaa za nyumbani, mfano mimi nina line ya TTCL ambayo intaneti yake ni ya kasi zaidi inaniwezesha kufanya kazi zangu kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kuendesha Akaunti zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii” alesema Shilole.
 
TTCL imedhamiria kuwa Shirika kinara katika utoaji wa huduma za Mawasiliano Nchini, nafasi iliyokuwa nayo hapo awali. Kupitia maboresho makubwa inayoyafanya, TTCL imeweza kutoa gawo la Tsh Bilioni 1.5 mwaka huu wa fedha na kuahidi kuongeza kiasi cha gawio katika miaka inayofuata sambamba na kuongeza uwekezaji katika teknolojia za kisasa, ubora wa huduma na ushiriki wa TTCL katika kutoa ajira kwa Watanzania na kusaidia shughuli za kijamii.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mara baada ya kusaini mkataba huo. Mkataba huo ambao pia msanii Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaini na kampuni hiyo, waasanii hao wameingia makubaliano kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba.

Msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba.

No comments:

Post a Comment

Pages