Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenesta Mhagama (kulia), akiwakabidhi Meneja Uhusiano Biashara za serikali wa benki ya NMB,Christabel Hiza (kushoto) na Meneja Uhusiano Mwandamizi idara ya Kilimo biashara,Oscar Rwechungura kombe la ushindi wa kwanza taasisi za fedha kwenye kilele cha maonesho ya Kilimo Kanda ya Kaskazini Nanenane Themi mkoa wa Arusha. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA
MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB imetoa mafunzo kwa
zaidi ya vyama vya msingi 1, 000 vya Ushirika wa Wakulima (AMCOS),
yanayohusu kilimo na utunzaji fedha ndani ya mwaka mmoja, yenye lengo la
kuboresha sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza katika madhimiso ya
kilele cha Sikukuu ya Wakulima ‘Nane Nane’ mkoani Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji
wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema benki yake imemaua kusaidia kuboresha
sekta ya kilio kutokana na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa
nchi na pia kuboresha uchumi wa wakulima.
Alisema kuwa, mafunzo hayo ambayo yanaendelea sehemu
mbalimbali nchini, yanatarajiwa kuwafikia wakulima wengi zaidi kupitia
vyama vya ushirika na hivyo vitawezesha kuboresha kilimo na kuleta mabadiliko
ya kiuchumi katika ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Bussemaker aliongeza kuwa, sekta ya kilimo ni
uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 70, hivyo
inapaswa kuboreshwa ili kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi.
Alisisitiza kuwa unatakiwa ushirikiano wa
wadau mbalimbali wa mendeleo ili kusaidia sekta ya kilimo kukua kwa haraka na
kuleta tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla na kuwa ikiachiwa serikali peke
yake haitaweza kuleta mabadiliko hayo kwa haraka.
Alibainisha ya kwamba benki yake inaamini kuwa
sekta ya kilimo ina uwezo mkubwa wa kuleta mapinduzi ya kweli katika
uchumi endapo kilimo kitaboreshwa nchini na kwamba itakuwa na mchango mkubwa
katika kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa viwanda.
Bussemaker alisema kuwa mbali na mafunzo
hayo benki yake imekwishatumia zaidi ya Sh. bilioni 100 katika kuboresha sekta
ya kilimo nchini kwa kutoa mikopo mbalimbali pamoja na huduma zingine za kifedha
kwa wakulima.
“Ndani ya miaka michache ijayo, tunatarajia kutumia
kiasi cha Sh. bilioni 500 katika sekta kuwezesha shughuli za kilimo
katika mnyororo mzima wa thamani, hivyo nawaomba wakulima kutokata tamaa na
kilimo kwani benki yao ipo pamoja nao katika kuhakikisha inaleta
mageuzi ya kilimo kwa manufaa na mendeleo ya wakulima na taifa kwa ujumla”
alisema Bussemaker.
Aliwataka wakulima kutumia Benki ya NMB ili kuleta
mageuzi chanya katika kilimo na kuinua uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa
kati kwa kuzalisha malighafi zaidi ndani ya nchi ambazo zitatumika katika viwanda
vilivyopo nchini kwa kuwa mkulima akilima zaidi viwanda vinapata malighafi
zaidi.
No comments:
Post a Comment