HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2018

NSSF TABORA ILIYOSHIRIKI MAONYESHO YA NANENANE 2018

WATENDAJI wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) wametakiwa kwenda walipo wananchi ambao hawako katika sekta isiyo rasmi ili wawaze kutoa elimu ambayo itawezesha kujiunga na hatimaye wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kutembelea banda la NSSF wakati  wa kilele cha maonesho ya nane nane kwa kanda ya Magharibi yalifanyika mjini Tabora.

Alisema mpango huo unachama wa hiari na sekta binafsi unatakiwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamejiari wenyewe ili nao wajiunge kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni kupitia michango ambayo watakuwa wakichangia kila mwezi wakati wakiwa na nguvu.

Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga alisema jambo hilo ni zuri kwani tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 hakuna Mfuko ambapo uliweza kumjali mtu asiye katika sekta isiyo rasmi na kuongeza kuwa ni jukumu la Watumishi wa NSSF kwenda kwao ili wawahimize waweze kuchangamkia fursa hiyo ambayo ni msaada kwao.

“Msisubiri wananchi wawafuate bali mnatakiwa kuwafuata walipo katika shughuli zao na kuwaelimisha ili hatimaye wengi wajiunge”alisema.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Mfuko huo umekuja na mpango ambao umjali Mtanzania wa kipato cha chini naye kupata kiunua mgongo akichangia kwa miaka isiyopungua 15 kama alivyo mtumishi mwingine.

Alisema mpango huo unawahusisha watu kama vile mamalishe, boda boda, muuza karanga na wengine wote ambao walikuwa hawana mifuko ya kuchangia sasa wanatakiwa kujiunga na NSSF ili hatimaye kunufaika wakiwa wazee.

Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Nour Aziz aliwataka watu ambao sio waajiriwa katika sekta rasmi kuchangamkia kwani NSSF inawakinga na majanga ya kiuchumi na kijamii kwa kutoa mafao kulingana na taratibu zilizowekwa na hivyo kumwezesha kufanyakazi bila hofu kwa kuwa wanamwezesha kujenga maisha yao ya sasa na baadae.

Alisema kuwa kupitia michango ya shilingi 20,000 ambazo wanachama atatoa kila mwezi, akifikisha miezi mitatu na kuendelea atapata Kadi ya Matibabu ambayo itamwezesha yeye na watoto wake wanne na wenza kupata matibabu na huku akiba yake ikiwa palepale.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrrey Mwanri (kushoto), akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi waati wa kilele cha kilelea cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane Kanda ya Magharibi Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga wakati walipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yaliyofanyika Agosti 8, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrrey Mwanri (kushoto), akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi waati wa kilele cha kilelea cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane Kanda ya Magharibi Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati walipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yaliyofanyika Agosti 8, 2018.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tabora, Nour Aziz (wa tatu kushoto), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga, wakati walipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yaliyofanyika Agosti 8, 2018.
 Ofisa Matekelezo wa NSSF mkoani Tabora, Victor Mbesigwe (kushoto), akitoa maelezo kwa mwananchi, Ngunda Shija, juu ya uanachama wa hiari na jinsi mwananchi kutoka sekta binafsi anavyoweza kujiunga wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Magharibi.
 Mtumishi wa NSSF Mkoa wa Tabora, Ester Mng'omba (kushoto), akimsaidia kujaza fomu ya kuwa mwanachama wa hiari dereva wa Bodaboda mara baada ya kutembelea banda la NSSF wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora.
Ofisa Matekelezo wa NSSF mkoani Tabora, Victor Mbesigwe (kushoto), akitoa maelezo kwa wananchi waliojitokeza katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Magharibi.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tabora, Nour Aziz, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafao yanayotolewa na NSSF, na kutoa rai kwa wananchi wa Tabora na Tanzania kwa ujumla kujiunga na NSSF ili kuweza kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
  Meneja wa NSSF Tabora, Nour Aziz (kushoto walioka mbele) na wafanyakazi wakiwa kwenye maonyesho ya Nanenane kwenye viwanja vya Fatma Mwassa.

No comments:

Post a Comment

Pages