Na Talib Ussi, Zanzibar
Waandishi wa Habari
Visiwani Zanzibar wameshauriwa kuifuatilia na kuiandikia Miradi ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya
kuona faida zake na pia kuibua changamoto zinazojitikeza kwa maslahi ya Umma.
Akizungumza katika mafunzo ya siku moja yaliondaliwa
kwa pamoja kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Shirika la Umoja wa
Mataifa (UN) na kushirikisha waandishi
20 kutoka Unguja na Pemba kwa niaba ya
Ofisi ndogo UN Zanzibar, Mtaalamu wa Uratibu wa Shirika hilo Bi Aine Mushi
alieleza kuwa wanahabari ni nguzo muhimu sana katika kufikia malengo ya miradi
yao.
Alisema kuwa UN inadhamira njema kushirikiana na
vyombo vya habari ili kuhakikisha vinaelewa na kuandika habari sahihi kuhusiana
na miradi ya shirika hilo.
Alieleza kuwa tarehe 28
mwezi huu UN itazindua Pragram maalumu ya pamoja Zanzibar(Zanzibar Joint
Proram) ZJP ambayo itahusisha mashirika
9 ya Umoja huo ambapo Rais wa Zanzibar na Baraza la Mapinduzi atakuwa Mgeni
Rasmi.
Alielaza kuwa Program
hiyo itajielekeza kwenye maeneo manne ya maendeleo ambayo ni Kupunguza Vifo vya
uzazi, Ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa wanawake
kupitia zao la Mwani na Uratibu wa Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya
Dunia.
“Ili kufanikiwa kwa miradi
hii basi ushiriki wa waandishi wa habari ni muhimu sana kwani nyinyi ndio
mtakao Ueleza umma nini kimefanyika na nini bado” alieleza Bi Aine.
Mafunzo hayo yalikuwa na
lengo ya kujenga Uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika kwa usahihi kazi
zinazofanywa na UN na mashirika yake katika eneo la Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya
kikosi kazi cha Mawasiliano cha UN (UNCG), Mchambuzi wa Mawasiliano wa UNFPA,
Warren bright alisisitiza umuhimu wa Vyombo vya habari katika miradi ya Umoja
huo na kueleza kuwa Vyombo vya habari ni mshirika muhumu katika kazi zao.
“kushirikiana na vyombo
vya habari ni suala muhimu kwa UN hapa Zanzibar kwani wao ndio wanaoweza kupaaza sauti na kuzifikia
jamii na kutangaza mafanikio na changamoto za kazi zetu ili na sisi kujiweka
sawa” alieleza Bright.
Katibu wa TEF, Neville
Meena alisema kuwa Jukwaa hilo limekuwa likifanyakazi na UN kwa miaka mitano
sasa na kufahamisha kuwa ushirikiano huo sasa unalenga kuimarisha shughuli zote
zinaztekelezwa na pande mbili hizo.
Sambamba na hilo Meena
aliwaomba wanahabari hao walioshiriki Mafunzo hayo kuyafanyiakazi kwa vitendo
yale yoote waliyoyapata kwa maslahi ya Taifa.
Shirika la Umoja wa
Mataifa (UN) kwa upande Zanzibar linatekeleza miradi Zaidi ya 270.
No comments:
Post a Comment