HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 07, 2018

WAZIRI DKT.KALEMANI AIPA "KONGOLE" TANESCO, MWEKEZAJI AIFAGILIA SERIKALI

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (kulia), na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kamel Group, wamiliki wa Kamel Industrial Estate, Bw.Gagan Gupta, wakitembelea eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate huko Bagamoyo Mkoani Pwani Agosti 6, 2018.

NA MWANIDHI WETU
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na mwekezaji wa Kampuni ya Kamel Group, Bw. Gagan Gupta, wamelipongeza Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kwa kuharakisha uwekaji umeme mkubwa kwenye eneo la EPZA Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Pongezi hizo zimetolewa Agosti 6, 2018 wakati Mhe. Dkt. Kalemani alipofika kwenye eneo hilo la uwekezaji viwanda (Kamel Industrial Estate), lililoko kandokando ya Barabara ya Bagamoyo Wilayani humo.
“Niipongeze TANESCO kwa sababu imechukua muda mfupi sana tangu ulipolalamika, takriban miezi miwili kazi ya kufikisha umeme hapa imekamilika, na ilikuwa ni kazi kubwa, umeme wa kiwanda hiki ulikuwa una–share na watumiaji wengine wengi, 33kV uki-share na watu wa Bagamoyo, watu wa Tegeta, kwa mtu wa kiwanda usingekutosha.” Alisema.
Alisema TANESCO baada ya kupokea malalamiko hayo kazi ya kuongeza kiasi cha umeme kwenye kiwanda hicho ilianza kwa kufunga mitambo hapo hapo kiwandani, ambapo umeme ulivutwa kutoka unapoanzia Mkoa wa Pwani kuelekea Bagamoyo.
“Tumeamua kukuwekea laini yako peke yako, kutoka pale Mkoa wa Pwani unapoanzia na kuleta umeme hapa, na kisha tumeuingiza kwenye transfoma yako, tumeingiza 33kV kwa ajili yako yenye uwezo wa kutumia Megawati 22, ingawa umetuambia mahitaji yako ni Megawati 20, sisi tumekuletea ziada ya Megawati 2 hivyo ni matumaini yetu sasa kero itapungua na uzalishaji utaongeza.”
Alisema ni matumaini ya Serikali kuwa kiwanda kitazalisha zaidi ya Mitungu 500 iliyokuwa ikizalisha kwa siku kwani hivi sasa umeme upo wa kutosha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Bw. Gagan Gupta alisema, amefurahi sana kupelekewa umeme wa kutosha moja kwa moja kwenye kiwanda chake na kwamba ameahidi kuwa uzalishaji mkubwa utafanyika ndani ya kipindi kifupi kijacho.
“Kwangu mimi leo ni siku ya kihistoria, Mhe. Waziri uko hapa ninakuahidi katika nia hii ya serikali ya kuweka uchumi wa viwanda, ninachoweza kusema, ongezeko la Megawati 20 moja kwa moja hapa kiwandani, ndani ya mwaka mmoja utakuta mabadiliko makubwa hapa.” Alitoa hakikisho Bw. Gupta.
Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
Mhandisi Mahende Mgaya, (Kulia), akimpatia maelezo Mhe. Dkt. Kalemani kwenye eneo ambalo TANESCO imetengeneza laini pekee ya kuelekea moja kwa moja eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate.
Dkt. Kalemani akizungumza na Bw. Gupta alipowasili kwenye eneo hilo.
Mhe. Dkt. Kalemani, akimpongeza Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mgaya. Kulia ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu.

No comments:

Post a Comment

Pages