WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa
kuchora ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho ambayo itatumika
kwenye ujenzi wa nyumba za utamaduni wa makabila mbalimbali nchini.
Amesema
uamuzi huo utarahisisha watu kufika kwa urahisi katika nyumza za
tamaduni za mikoa yao kwa kuwa watakuwa wanatumia ramani Tanzania.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Agosti 4, 2018) wakati akizungumza
na wakazi wa mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya
Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho, jijini
Dar es Salaam.
“Kwa
kutumia ramani hii kila mkoa utaweza kufika kwenye eneo lake kwa
kutumia ramani ya Tanzania na mkoa wa Lindi tayari umeshaoneshwa eneo
lake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba inayozingatia utamaduni wetu,”
alisema.
Alisema
kwa tamaduni za makabila ya mkoa wa Lindi nyumba zote hujengwa kwa
udongo na kuezekwa kwa makuti upande wa maeneo ya pwani ya upande
mwingine huezeka kwa nyasi, ambapo aina zote zitajengwa ili kuwakilisha
tamaduni za wakazi wa mkoa huo.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi ambao kwa mwaka huu ndio
waandaaji wa tamasha hilo wadumishe mshikamano wao ili waweze kutimiza
malengo waliyojiwekea katika kuboresha maendeleo.
Alisema
katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 26 hadi 29
wahakikishe wanapeleka kila kitu ambacho kinahusiana na utamaduni wa
mkoa huo ili kuwawezesha Watanzania wengine wajue kama vyakula na mavazi
.
Pia
alishauri wawepo wazee wenye kujua historia ambao watasimulia utamaduni
wa wananchi wa Lindi pamoja na kutambulisha ngoma zao za utamaduni.
“Halmashauri zote za mkoa wa Lindi zitumie fursa hii kutangaza vivuti
vya utalii vilivyopo na Kilwa walete mtu atakayeelezea kuhusu magofu,”.
Waziri
Mkuu alisema tamasha hilo ni muhumu kwa sababu utamaduni ulianza
kufifia nchini kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia jambo ambalo
lingeweza kuuondoa katika kumbukumbu, hivyo aliwashauri siku ya tamasha
hilo wavae nguo za kitamaduni kulingana na kabila husika.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu
wa Mkoa Bw. Godfrey Zambi kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni
pamoja na kusimamia vizuri mwenendo wa zao la korosho.
Awali, Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla alisema mwaka
huu Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania linawakilishwa na jamii kutoka
mkoa wa Lindi na kwamba anatumaini watafanya vizuri kwa kuwa uwezo na
nia wanayo.
Profesa
Mabula alisema mwaka 1994 Bodi ya Makumbusho ya Taifa ilianzisha siku
ya utamaduni ili kutoa fursa kwa jamii mbalimbali nchini kuonesha
utajiri walionao katika tamaduni zao na ufanisi wa siku hiyo unatokana
ushirikishwaji wa wanajamii husika.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 5, 2018.
No comments:
Post a Comment