Wadau wakifuatilia
uwasilishwaji wa mwongozo wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta
binafsi kupitia mabaraza ya biashara ya
Mikoa na Wilaya katika kikao kazi kilichoandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara
(TNBC) tarehe 25 Septemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Wadau wakifuatilia kwa
karibu uwasilishwaji wa mwongozo wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta
binafsi katika kikao kazi kilichoandaliwa
na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano
wa Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 25 Septemba,2018 Jijini Dar es Salaam.
Mshauri Mwelekezi kutoka
Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Prof. Honest Prosper Ngowi akiwasilisha
majadiliano kwa wadau wakati wa kikao kazi cha Baraza la Taifa la Biashara
kujadili Mwongozo kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa ngazi ya Mikoa na
Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar
es Salaam tarehe 25 Septemba, 2018.
Mwakilishi wa Kaimu Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Willy Magehema akifafanua jambo
wakati wa majadiliano ya mwongozo baada ya kuwasilishwa na Mshauri mwelekezi
katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu JijininDar es Salaam tarehe 25
Septemba, 2018
Patrick Mavika kutoka
Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha
majadiliano ya mwongozo kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mabaraza
ya biashara ya Mikoa na Wilaya kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya
Waziri Mkuu Dar es Salaam tarehe 25 Septemba, 2018. Kulia Mwakilishi wa Kaimu
Katibu Mtendaji wa TNBC Willy Magehema.
Dar es Salaam, Septemba, 25, 2018
Baraza la Taifa la Biashara
Nchini (TNBC) limeandaa mwongozo wa majadiliano utakaosaidia Sekta ya Umma na
Sekta Binafsi kupitia mfumo rasmi wa mabaraza ya biashara ya Mikoa na Wilaya nchini.
Hayo yamesemwa na Willy Magehema
kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwamba
lengo la mwongozo huo ni kuimarisha mahusiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
katika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii hasa zinazolenga katika kuwezesha
ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji nchini.
“Mwongozo huu utasaidia
kuleta tija na ushirikiano wa Sekta Umma na Sekta Binafsi katika kuinua mipango
ya maendeleo ya sekta Binafsi Nchini”, alisema Magehema.
Mwongozo huu unaeleza kutoa
maelekezo ya mambo muhimu ya kuzingatia katika Majadiliano kati ya Sekta ya Umma
na Sekta Binafsi. Dhumuni ni kuyaimarisha na kuyawezesha mabaraza ya Biashara
ya MIkoa na Wilaya yaweze kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Taifa kwa
kuelezea mambo yanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa Maandalizi ya
majadiliano;Uendeshaji wa majadiliano na baada ya majadiliano.
“Mwongozo huo utashirikisha
wadau kutoka katika sekta zote pale inapohitajika ili kutakua kero na
changamoto zinazojitokeza katika mabaraza ya biashara kama vile masuala ya
ukusanyaji kodi, miundombinu, Afya na mengine yote yanayohusu Sekta ya umma na
Sekta binafsi yataainishwa katika mwongozo huo” alisisitiza Magehema.
Pia mwongozo huo utatoa maelezo
ya kina ikielezea ni yapi ya Kufanya
na Kuepuka ili kuongeza ufanisi kwenye majadiliano kati ya Sekta Umma na
Sekta Binafsi.
Mapema: Wadau
walioshiriki katika kikao kazi hicho, wameeleza kuwa Baraza la Taifa la
Biashara liendelee kujenga uhusiano mzuri utakaojenga uaminifu kati ya Sekta ya
Umma na Sekta Binafsi, vilevile wakuu wa Mikoa na Wilaya watambue kuwa
maendeleo ya mabaraza ya biashara
yanaanzia katika mikoa yao na Wilaya zao kwanza.
TNBC pamoja na wadau wengine watapitia rasimu ya
mwongozo huo itauhakiki kwa kushirikiana
na wadau kwenye mikoa Tanzania bara na baadae kuwasilishwa katika kamati tendaji
ya baraza la Taifa la Biashara kwa ajili ya uhakiki wa mwisho kabla ya kuanza
kutumika.
Uandaaji wa mwongozo huu
umeratibiwa na TNBC kwa msaada wa mradi wa Local Investment Cimate (LIC )na
Enabling Growth Through Investment and Enterprise (ENGINE).
Imetolewa
na;-
Afisa Habari
Ofisi ya Waziri Mkuu
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment