Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu
(watatu kulia) leo akiongoza Matembezi ya Hiyari kuelimisha na kuhamasisha
Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyoanzia kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mohamed Kambi.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni
mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha
Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakipiga picha mbele ya bango lenye ujumbe kuhusiana na
ugonjwa wa Ebola la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mara baada ya
kumalizika kwa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia
ugonjwa huo usiingie nchini yaliyofanyika leo kwa kuanzia kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Kariamjee jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard
Mayongela akiongea na wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha
na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam kwa kuanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia
kwenye Viwanja vya Karimjee.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo
akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na
kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu
leo akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa udhibiti wa ugonjwa wa
Ebola usiingie nchini, baada ya kufanya Matembezi ya Hiyari yaliyoanzia kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu leo
akitembea mbele ya bango la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakati
wa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa
Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii
kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,
wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment