Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana
Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa neti ya mbu kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo
cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel
Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali
vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana
Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa dogoro kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha
yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel
Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali
vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa
Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana
Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa kitanda kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha
yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel
Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali
vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa
Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo.
Morogoro, Tanzania
Kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha huduma kwa wateja
imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Mgolole Orphanage
Center, Morogoro.
Msaada huo
ni pamoja na vitanda, neti, magodoro, deep freezer, chupa za chai, hot pot,
sukari, sahani, sabuni, nepi, pampers na toy za watoto vyote vikiwa na thamani
ya TZS 18 milioni.
Kutoa kwa
msaada huo ni muendeleo wa kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu ya
Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kukubali kutoa sehemu ya
mshahara wao ili kusaidi huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha
Mgolole cha Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel
Tanzania Adriana Lyamba alisema muda mrefu wafanya kazi wa Airtel kupitia
Airtel tunakujali imekuwa ikitembelea na kusaidia vituo mbali mbali vya yatima
ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada mbali mbali.
Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni
sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki
ambacho tumekuja kutoa leo hapa ni
kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko
pamoja nanyi na tunawajali sana, alisema Lyamba.
Naomba kutoa pongezi za dhati kwa wafanyakazi wenzangu wa Airtel
kwa kukubali kutoa sehemu ya kipato chao na leo tumeweza kufika hapa. Lakini
zaidi napongeza uongozi wa kampuni yetu kwa kukubali na kuridhia programu yetu
hii hapa ya Airtel Tunakujali ambayo imekuwa ikituleta karibu na Jamii
inayotuzunguka, alisema Lyamba.
Tunayo furaha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako kwenye
kituo hiki na dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto wanaoishi
kwenye mazingira mangumu na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya
Airtel, aliongeza Lyamba.
Kwa upande wake, Makamu Mama Mkuu
wa kituo cha Mgolole Sista Valeria Mnyanzaga alisema ni furaha kwa kampuni
kubwa ya Airtel kuguzwa na maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hiki na
hatimaye kuja kutoa msaada na kutuunga mkono.
Najua kuna vituo vingi vya
mayatima hapa nchini kama sisi hapa. Kuamua kuja kuwa na sisi ni Baraka kubwa
kwetu. Nachukua fursa hii kuwapongeza wote kwa kile mlichotoa ambacho mnaweza
kudhani ni kidogo lakini kinaleta matumaini makubwa kwetu na hasa kwa hawa
watoto. Naomba kuwakaribisha tena hapa na sio lazima kuja kutoa msaada, lakini
mnapokuja kujumuika na hawa watoto wanapata faraja kubwa na kujisikia kama
sehemu ya Jamii kwani wengi wao hapa hawajawahi kuona Wazazi wao, alisema
Mnyanzaga.
Kituo cha Mgolole ambacho
kiliazishisha mwaka 1937 kimekuwa kikilea na kusomesha watoto yatima kutoka
sehemu mbali mbali za Tanzania. Mmoja wa wanufaika wa kituo hicho ni Sebastian
Alphonce ambaye amekulia na kusomea kwenye kituo hicho. Kama mnavyoniona mimi
nimekuwa mzee kwa sasa. Lakini nimekulia na kusomesha na kituo hiki. Hatimaye
nikawa Afisa polisi na kustaafu mwaka 2016 kwa mujibu wa sharia zetu. Hata
hivyo, baada ya kustaafu nikaona ni busara kuja kuendelea kukaa na hawa wototo
ili kutambua na kuelewa kuwa yatima sio mwisho wa maisha, alisema Aphonce.
Natoa shukrani za dhati kwa kituo
cha Mgolole kwani bila kituo hiki sijui leo ningekuwa wapi. Lakini zaidi ni kwa
kampuni ya Airtel ya kwa msaada huu. Kutoa msaada huu ndio kunawafanya hawa
watoto wajione ni sehemu ya Jamii kwani wengi hawajawahi kuwaona Wazazi wao
kabisa, alisema Alphonce.
No comments:
Post a Comment