HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2018

KAMPUNI YA KILUWA GROUP YAWATAMBULISHA WADAU WAKE WA UWEKEZAJI WA VIWANDA KWA MKUU WA MKOA WA PWANI

Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa alipokuwa akiwatambulisha Wadau wake wa uwekezaji kutoka nchini china,waliofika Oktoba 29,2018  kumtembelea na kujitamulisha ofisini kwake ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong akiwa ameambatana na Wenzake Wane.Kampuni hiyo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China. 
Meneja wa Kampuni ya Kiluwa Group Ndugu Madoweka pichani kulia akifafanua zaidi kwa lugha ya Kichina, kilichokuwa kikizungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo kwa Wawekezaji hao waliofika nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya Kiluwa Group,kutafuta fursa za uwekezaji wa viwanda katika bidhaa mbalimbali za ngozi
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong akiwa ameambatana na Wenzake Wane (hawapo pichani),akiushukuru uongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Kampuni ya Kiluwa Group kwa mapokezi mazuri kufuatia ujio wao wa kutafuta fursa za uwekezaji kupitia kampuni yao inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China,pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group Bi.Naima Kiluwa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na ugeni wake uliomtembelea Ofisini kwake Oktoba 29,2018 na kuzungumza nae mambo kadhaa katika suala zima la uwekezaji katika mkoa wa Pwani,wakiwa na mwenyeji wao Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa .
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akiangana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong inayojishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya utamulisho

No comments:

Post a Comment

Pages