*Awasisitiza watumishi wa umma wawe waadilifu na waaminifu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema vitendo vya udokozi wa mali ya umma
havitavumiliwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.
John Magufuli, hivyo amewataka watumishi wawe waadilifu na waaminifu
wanapotekeleza majukumu yao.
Ameyasema
hayo leo (Alhamisi, Oktoba 11, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika mkutano uliofanyika kwenye
ukumbi wa halmashauri hiyo akiwa katika ziara mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema Serikali haitamvumilia watumishi wa umma ambaye si
muadilifu, mvivu na wala rushwa hawana nafasi, hivyo ni lazima wajibike
na ambao watashindwa kutekeleza majukumu yao watapa shida kwenye
Serikali hii. “Hakuna mchezo kwenye Serikali hii, watumishi wa umma
wanapaswa kulitambua hili.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewataka watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza
majukumu yao kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa kwenye Ilani ya uchaguzi
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015/2020.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wahakikishe wanapanga ratiba ya
kwenda kuwatembelea wananchi hususani waishio vijijini na kushirikiana
nao katika kutatua kero zinazowakabili si kukaa ofisni.
Waziri
Mkuu amesema kila mtumishi kwenye idara yake anapaswa kwenda kwa
wananchi, kama ana siku tano za kufanyakazi kwa wiki basi siku tatu
azitumie kwenda kwa wananchi kutatua changamoto zao na kama ana siku
sita, siku nne azitumike kuwafikia wananchi.
Akizungumzia
kuhusu idara ya kilimo, Waziri Mkuu amesema Maafisa Kilimo wote
wanatakiwa kwenda vijijini kufanyakazi na si kubaki ofisini na alishatoa
agizo hilo alipokutana nao jijini Dodoma. “Wakulima huko vijijini
wanahangaika peke yao huku maafisa kilimo wamekaa ofisini.”
Waziri
Mkuu amewataka watumishi wa umma wazingatie itifaki, mipaka ya madaraka
yao pamoja na kuheshimu viongozi. Amesema hata kama ni mkuu wa idara
pia anapaswa kumheshimu mtumishi aliyekuwa chini yake.
Awali,Spika
wa Bunge, Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, aliishukuru
Serikali kwa kutatua kero mbalimbali ikiwemo changamoto ya ukosefu wa
maji pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mbande
hadi Kongwa ambapo aliomba ujenzi huo uendelee hadi Mpwapwa.
Aidha,
aliiomba serikali kugawa kwa vipande eneo la Rachi ya Taifa lililopo
wilayani hapo kwa wafungaji kwa kuwa limekuwa halitumiki. “Napendekeza
wananchi wapewe vitalu kisha wafuge kwa njia ya kisasa kwa kupatwa mbegu
bora. Hii itasadia kuzalisha bidhaa bora za nyama na maziwa pamoja na
wananchi kupata ajira.”
NayeMkuu
wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi aliishukuru Serikali kwa kuwapatia
fedha za kutekeleza miradi mbalimbali wilayani humo, hadi sasa
wameshapokea zaidi ya sh. bilioni tatu kwa ajili ya miradi ya maji.
Kuhusu
upatikanaji wa dawa kwenye wilaya hiyo alisema umefikia zaidi ya
asilimia 90 na wananchi wanapata huduma ya matibabu kwa ubora.
“Pia
Kongwa hakuna njaa. Tumeweza kuhamasisha kilimo cha mtama kwenye vijiji
89 ambapo Mbunge (Ndugai) alitoa sh. milioni saba kwa ajili ya mbegu
ambapo sasa tumeweza kufikia ziada ya tani laki mbili.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge alisema
mafanikio ya Kongwa ni matokeo ya uwepo wa amani na utulivu kwenye eneo
hilo.
Hata
hivyo, alimuomba Waziri Mkuu baada ya rais kusaini sheria ya Dodoma
kuwa makao makuu ya nchi ni muhimu ikapewa kipaumbele pamoja na miji
mingine midogo inayozunguka jiji la Dodoma kupata fedha za kupima
maeneo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
ALHAMISI, OKTOBA 11, 2018.
No comments:
Post a Comment