HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2018

CRDB: NSEKELA MBOBEVU SEKTA YA BENKI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akizungumza na wakurugenzi, mameneja, wafanyakazi wa benki hiyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akizungumza na wakurugenzi, mameneja, wafanyakazi wa benki hiyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.
Abdulmajid Nsekela, akiteta jambo na Ally Laay.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB.

 Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa CRDB Bank.
 Mkutano ukiendelea.
 Wakurugenzi wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Ally Laay akiwa na Abdulmajid Nsekela.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Mwenyekiti wa Bodi.
 Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela na Mwewnyekiti wa Bodi, Ally Laay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela baada ya kutoa hotuba yake.
 
NA IRENE MARK
 
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay amesema Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, ni mbobevu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 wa masuala ya kibenki.

Kwa sababu hiyo, bodi yake haikuona sababu ya aliyekuwa kuendelea kuwahudumia wakurugenzi wawili ambao ni Dk. Charles Kimei aliyemwachia madaraka, Nsekela.

Akizungumza na wakurugenzi, mameneja, wafanyakazi wa benki hiyo na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati wa kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB.

“Bodi iliamua kumpumzisha Dk. Kimei kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni kuendeleza misingi ya utawala bora na maadili ya kazi. Pili ni kwa sababu ndugu Nsekela ni mbobevu mwenye zaidi ya miaka 20 kwenye sekta ya benki hivyo hakuhitaji kushikwa mkono kuelekezwa.

“…Ndugu Nsekela alianza kazi za kibeki mwaka 1997 akiwa mshauri wa mikopo wa benki ya CRDB mkoani Iringa,” alisema Laay na kuongeza kwamba kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Nsekela alikuwa Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wakati wa Benki ya NMB.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa bodi, uongozi wa benki ya CRDB unathamani mchango mkubwa wa Dk. Kimei kwa benki na uchumi wa taifa kipindi chote cha uongozi wake.
Akiishukuru Serikali na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kumuamini, Nsekela aliahidi kufanyakazi kwa weledi na ubunifu utakaoongeza ubora wa huduma za benki hiyo.

“Kwa kushirikiana na wakurugenzi na viongozi waliopo ninaahidi tutafanya maboresho kwa kutilia mkazo maeneo ya mifumo na taratibu za utoaji wa mifumo, kuongeza weledi wa wafanyakazi, kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa na kukuza biashara katika sekta zote,” alisema Nsekela.

Alisema CRDB imeweka malengo la kufikisha huduma kwenye wilaya zote hapa nchini ifikapo mwaka 2022 huku akiahidi kuongeza thamani ya benki hiyo kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages