*Ni kutokana na biashara za magendo zinazoendelea wilayani humo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amechukizwa na biashara za magendo zinazoendelea katika wilaya ya
Kyerwa mkoani Kagera, hivyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo wajipime
wenyewe.
Pia,
Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa
wa Kagera Bw. Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika
mpaka wa Mulongo Bw. Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara
za magendo.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumanne, Oktoba 9, 2018) wakati akizungumza na
viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya
kikazi ya siku nne mkoani hapa kilichofanyika mjini Bukoba.
“Biashara
za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani
hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe,
mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na
butura.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo
ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za
magendo na butura zinafanyika na hakuna kiongozi wanaochukua hatua.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu alimtaka Meneja wa TRA asiwahamishe watumishi wabovu kutoka
kituo kimoja cha forodha na kuwapeleka kingine kwa kuwa huko
wanakowapeleka wanakwenda kuendeleza biashara za magendo na kuikosesha
Serikali mapato.
Alitolea
mfano mtumishi wa mamlaka hiyo Bw. Mtei ambaye alihamishiwa kituo cha
Mulongo akitokea kwenye kituo cha Mtukura kilichopo katika mpaka wa
Tanzania na Uganda kwa tuhuma za kuchua rushwa na kushirikiana na
wafanyabiashara wa burura.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu alisema mtumishi huyo tayari alishapewa barua ya
uhamisho kwenda katika kituo cha forodha cha Rusumo miezi minne
iliyopita hadi sasa hajahama na anaendelea na biashara za magendo ambapo
Agosti 5, mwaka huu anadaiwa kupitisha mzigo wa magendo uliobebwa
kwenye gari aina ya fuso yenye za usajili T 957 AXF mali ya Erasto Muga.
“Meneja
TRA msimamishe kazi Bw. Mtei leo (jana) hatuwezi kuwa na watumishi
wabovu alafu nyie mnawahamisha vituo ili wakaendelee kuharibu eneo
lingine. Mnajua mkakati wa Serikali hii ni kudhibiti rushwa hivyo
hatuwezi kuvumilia suala hili.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu alimuagiza Meneja wa TRA wa mkoa wa Kagera Bw. Ntogha
afanye ukaguzi kwenye vituo vyote vya forodha katika mkoa huo pamoja na
kuongeza idadi ya watumishi na kudhibiti vitendo vya rushwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, SEPTEMBA 10, 2018.
No comments:
Post a Comment