HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 08, 2018

Halotel yaadhimisha miaka mitatu ya huduma

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda (kulia), akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la Longa Tusonge. Kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda (kulia) , akionyesha baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa wateja wenye mawazo bora mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la Longa Tusonge. Kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias
 Msaidizi wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias ( kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la “Longa Tusonge”. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano.
 
 NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuadhimisha miaka mitatu ya utoaji wa huduma nchini, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel, imetangaza mpango wa kutoa zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo chanya katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja.

Mpango huo uliopewa jina la ‘LONGA TUSONGE,’ pamoja na faida zingine una lengo la kuwashirikisha wateja wote pamoja na wafanyakazi wa Halotel katika kufanya maboresho ya utoaji huduma mbalimbali kupitia mawazo yao wakati huu wanapoadhimisha miaka mitatu ya huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, alisema kuwa, mkakati huo ni sehemu ya kuthamini mchango mkubwa wanaoutoa wateja wao.

Semwenda alisema tangu kuingia kwa huduma za mtandao huo wa Halotel, wamekuwa wakipata matokeo mazuri ya wateja wake wanaondeelea kutumia huduma zake mbalimbali hadi wakati huu ambapo wanakuja na ‘LONGA TUISONGE.’

Kupitia mpango huo, wateja wa mtandao huo wanapewa nafasi ya kutoa mawazo yao mbalimbali ya kuboresha huduma za Halotel, ambayo baadae yatachujwa na kwa yale yatakayokidhi matakwa yatapitishwa na kuwa huduma rasmi ndani ya mtandao huo.
“Hii fursa kwa wateja wetu walioko nchi nzima katika kutambua na kuthamini mchango wao ambao wamekuwa wakituunga mkono tangu tuanze kutoa huduma za mawasiliano hapa nchini. 

“Lengo letu ni kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora za mawasiliano zinazotokana na mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia Mtandao wa Halotel,” alisema Semwenda.

Alisema zawadi hizo zitatolewa kwa wateja watakaotoa mawazo bora kupitia mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo, namba ya huduma kwa wateja, maduka ya Halotel yaliyopo nchi nzima, pamoja na barua pepe (callcentre@halotel.co.tz). Zawadi zitakazotolewa ni pamoja na simu za smatiphone, muda wa maongezi na fedha Taslimu.

No comments:

Post a Comment

Pages