Dar es Salaam Oktoba 8, 2018: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia yake ya Castle Lager, imemualika mmoja ya wachezaji bora barani Afrika Samuel Eto’o kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-Side utakaojengwa Oysterbay, Dar es Salaam. Uwanja ambao baada ya kukamilika utakuwa wazi kwa wananchi kucheza.
Nyota huyo ambaye kwa sasa anasakata kabumbu huko Qatar anatarajia kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam Oktoba 10 saa tisa na nusu mchana na kupokewa na mwenyeji wake TBL kupitia Bia yake ya Castle Lager.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alisema kuwa, nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na ufukwe wa Coco.
Alisema, TBL kupitia bia yake ya Castle Lager imeamua kujenga uwanja huo kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii ya watanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwaunga mkono kibiashara.
Lakini pia akasema kuwa, lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika soka hilo ambalo kwa sasa linachezwa kimataifa. Lakini pia kutoa fursa kwa watanzania ambao hawajawahi kumuona Eto’o.
“Sisi sote huwa na ndoto ya kupata nafasi ya kuwaona wachezaji wa kimataifa, haswa wale wenye majina makubwa kama E’too. Castle Lager ina furaha kubwa kufanya ndoto hii kuwa kweli kwetu sote kwa kutuletea Mchezaji huyu mwenye hadhi ya kimataifa hapa nyumbani,” alisema Kikuli.
Alifafanua kuwa, mapema mwaka huu, TBL kupitia bia yake Castle Lager, iliendesha mashindano ya soka ya Castle Lager 5-A-Side kupitia mfumo wa bonanza na kupata mshindi ambaye alikwenda kushiriki mashindano hayo ngazi ya kimataifa Zambia.
“Tulifanya mashindano hayo na sasa tumeona kuna umuhimu kuwa na uwanja ambao utatumika bure kwa watanzania katika kukuza vipaji vya mchezo huu, hatimaye tupate wawakilishi wazuri kimataifa kwa miaka ijayo. Mashindano haya yanafanyika kila mwaka ambapo Tanzania tumeanza mwaka huu,” alisema Kikuli.
Akizungumza katika hafla hiyo, mchezaji mkongwe wa soka nchini, Ivo Mapunda, ambaye pia ni balozi wa Castle Lager, alisema kuwa anaamini uwepo wa Eto’o nchini itakuwa chachu kwa watanzania kushiriki katika mchezo huo.
Alisema kuwa jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Castle Lager katika kukuza michezo hazina budi kufuatwa na wadau wengine wa michezo katika kukuza vipaji nchini.
Aliwataka wakaazi wa Dar es Salaam na vitongoji vya jirani kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ambapo watapata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu na Eto’o, akisisitiza kuwa nafasi kama hizo hupatikana mara chache sana.

No comments:
Post a Comment