Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mlezi wa Mtandao wa Vikundi
vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Stephen
Mashishanga wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
kumwakilisha Rais, John Pombe magufuli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya
MVIWATA, Oktoba 3, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
Dkt. Stephen Kebwe. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya
Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwenye uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu unga na bidhaa
mbalimbali zinaotokana na zao la soya kutoka kwa Julie Bwire wa Mvomero
(kushoto) kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao
wa Vikundi vya Wakulima Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro, Oktoba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa
uyoga, Maria Shindika wa Mvomero (kulia) kabla ya kuhutubia
katika Maadhidhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima
(MVIWATA) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Oktoba 3,
2018.
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya
Wakulima (MVIWATA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uswiss nchini,
Florence Tinguely Mattli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa
Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro,
Octoba 3, 2018.
No comments:
Post a Comment