Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akitia saini
kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma
kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
M. Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma
kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko, akimkaribisha Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt.
Mary M. Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi, mara baada ya kuripoti ofisini
kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akizungumza
na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara
baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akisalimiana
na mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Dodoma, Tanzania
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
M. Mwanjelwa (Mb) ameahidi kushirikiana na watumishi wa ofisi yake kupanga
mikakati endelevu itakayowezesha kutoa huduma bora kwa umma na kuhakikisha ofisi
hiyo inakuwa na mtazamo chanya katika kuwahudumia wananchi.
Dkt. Mwanjelwa
ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini
kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Dkt. Mwanjelwa ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wa ofisi
yake kwani kila mtumishi ana mchango na
umuhimu wake katika kuboresha utuoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri
mwenye dhamana ya utumishi na utawala bora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe.
Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018
na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 14 NOVEMBA,
2018
No comments:
Post a Comment