HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2018

MSHINDI WA GARI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA' AKABIDHIWA GARI ALILOSHINDA

Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya mshindi wa kwanza wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. Julitha Kilawe . Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba. Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe,(katikati) akionyesha ufunguo wa gari alilojishindia baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia)mwingine pichani Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( mwenye shati jeupe) akimfungulia gari na kumuelekeza jinsi linavyotumika Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe. 

Na Mwandishi Wetu
 
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia droo ya kwanza ya promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ leo amekabidhiwa rasmi gari lake katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam. 
 
 Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa gari lake Julitha Kilawe, alisema “Ninayo furaha kubwa kwa kujishindia gari kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa, mpaka siamini macho yangu, naishukuru TBL kwa kuniwezesha kupata usafiri huu”. 

Kilawe alisema gari hilo atalitumia kwa usafiri wa kwenda kazini na shughuli nyinginezo za kifamilia na aliwataka wateja wa bia kuchangamkia promosheni hii kutoka TBL ambayo imelenga kuboresha maisha ya wateja wake. 

Akiongea wakati wa kumkabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo na kutoa wito kwa wateja wote nchini kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID. 

 “Mshindi wetu wa kwanza kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa ameshapatikana na leo ndio amekabidhiwa rasmi gari lake. Natoa wito kwa wateja wetu popote walipo kuendelea kushiriki promosheni hii ya miezi mitatu bado kuna magari 2 kwa ajili yao na zawadi nyinginezo nyingi”, alisema Tarimo. 

Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. 

“Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’ 

Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. 

Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz

No comments:

Post a Comment

Pages