Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akitoa hundi ya shilingi
Milioni 3.5 kwa kikundi cha Perfect Group kinachotengeneza chaki Mnaipaa
ya Sumbawanga.
Rukwa, Tanzania
Mkurugenzi wa Manispaa
ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya amevihakikishia ajira na masoko vikundi 21 vya
vijana wanawake na walemavu kutoka katika ofisi ya halmashauri hiyo ili
kuongeza chachu ya maendeleo ya viwanda na kuongeza ajira na hatimae kuinua
vipato vya vikundi hivyo ili kuweza kutoa huduma ndani nan je ya Mkoa wa Rukwa.
Mtalitinya amesema kuwa
miongoni mwa vikundi vilivyopewa mikopo hiyo kuna kinachojishughulisha na
utengenezaji wa chaki, utengenezaji wa matofali, useremala na kufanya usafi
hivyo aliagiza kuwa shule zote zilizopo chini ya Ofisi yake kuhakikisha
wananunua chaki kutoka katika kiwanda hicho ili kukuza soko na mtaji wa kikundi
hicho pamoja na kuvitumia vikundi vya usafi katika kushiriki kuiweka manispaa
safi na kununua matofali kwaajili ya majengo ya taasisi za serikali katika
vikundi hivyo.
“Kiwanda cha chaki
ambacho tunakipa mkopo leo, tunaelekeza na ninaelekeza tena shule zangu zote za
manipaa tutanunua chaki zote kutoka katika kiwanda hichi kama utekelezaji wa
masoko, lakini pia kwa upande wa usafi hatutaajili wakala vikundi hivi vitapewa
kazi kwaajili ya usafi, wapo wanaofanya kazi za useremala na kazi nyingine
tutaendelea kuwatumia kwenye kazi zetu za ujenzi kama utengenezaji wa “Ma-grill”
kuhakikisha wanapata ajira na masoko na mitaji yao iweze kukua,”Alisema.
Mtalitinya aliyasema
hayo kwenye hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi 21 vya ujasiliamali iliyofanyika
katika ukumbi wa manispaa ya sumbawanga ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo
alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Kwa upande wake Mh.
Wangabo katika kuhakikisha masoko yanapatikana ndani ya mkoa aliziagiza
halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wananunua chaki kutoka katika kiwanda
cha kuzalisha chaki kilichopo manispaa ya sumbawanga ili kuthamnini na kukipa
uwezo kikundi hicho kufanya vizuri na kukuza uzalishaji na kuongeza ajira.
“serikali yetu ya wamu
ya tano inasisitiza uanzishwaji na uimarishwaji wa viwanda vyetu vya ndani ili
tupunguze kuagiza kutoka nje, sasa kama taifa tunalenga hivyo mkoa na wenyewe
uko hivyo hivyo, nilazima tuhakikishe kuwa bidhaa zetu za ndani tunapatia soko
ndani hapa hapa na kwa hali hiyo hizi chaki tunazotengeneza wenyewe katika mkoa
wetu ni lazima zitumike katika halmashauroi zetu zote,” Alibainisha.
Shilingi 70,590,000/= inatolewa leo hii
ili kuwezesha Vikundi 21 vya ujasiliamali
amba 13 ni vya Wanawake 7 vya Vijana na 1 cha Walemavu.vikundi hivi
vinajishughulisha na Usindikaji mafuta, chakula,vinywaji, Useremala,
Utengenezaji wa Chaki na ushonaji, ufumaji na utengenezaji wa Mabatiki na
Ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
No comments:
Post a Comment