NA TIGANYA VINCENT
BARAZA la Madiwani la
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limetaka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora
aitwe kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo
za kuwapiga na kuwaibia wananchi mali zao wakati wa Doria zao.
Madiwani hao wametoa
kauli hiyo leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya Baraza hilo kufutia hoja
iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Itojanda Alphonce Shushi ya uwepo wa
vitendo vya unyanyasaji wananchi vinavyofanywa na Mgambo.
Alisema Migambo hao kwa
kushirikiana na baadhi ya Askari wanapokuwa katika Doria wamekuwa wakiwapiga na
kuwanyanyasa na kuwahumiza baadhi ya watu.
Aliongeza kuwa baadhi
yao wamekuwa wakidiriki hata kuchukua mali za watu wanapowakata kwa kisingizio
cha kufanya Doria.
Naye Diwani wa Kata ya
Isevya Ramadhani Shabani alisema migambo hao badala ya kusaidia kupambana na
uhalifu wao ndio wako mstari wa mbele kuiba na kuwanyanyasa wananchi mitaani.
Alisema kuwa kazi yao
kubwa ni kupiga watu na kufukizana na madreva wa pikipiki na wakati mwingine
kuwabambikizia makosa.
Diwani wa Viti Maalumu
Kata ya Ifucha Rose Kilimba alihoji sababu zilizomfanya OCD kushindwa
kuhudhuria kikao Baraza la Madiwani wakati
siku zote amekuwa akihudhuria au akituma mwalilishi.
“Mheshimiwa Mwenyekiti
siku zote OCD anahudhuria vikao leo kwanini ameshinwa kuhudhuria na hata
kumtuma mwalilishi labda amejua kuwa tutamuuliza juu ya unyanyasaji unaofanywa
na hao migambo anawatumia” alisema.
Alisema kitendo hicho
kinasikitisha kwa walitaka wamweleze kero ambazo Migambo hao kwa kushirikiana
na baadhi ya askari wanasababisha.
elezea kusikitishwa
kwake na kitendo cha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora kushindwa kuhudhuria kikao
chao licha ya kumpatia taarifa kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi
ya askari wake na migambo.
Kwa upande wa Diwani wa
Kata ya Ng’ambo George Mpepo alimuomba Mstahiki Meya kusogeza mbele hoja hiyo
ili OCD apewe taarifa ya kuhudhuria kwa ajili maoani na maswali ya Madiwani kuhusu kero ambazo wanazipata wananchi kutoka na
askari na migambo wanapokuwa katika Doria.
Alisema baadhi ya
Migambo hao wanahistoria ya wizi na hivyo wanatumia fursa hiyo na Doria
kuchukua mali za wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora. Leopold Ulaya amemwagiza
Mkurugenzi Mtendaji wake kuhakikisha anamweleza Mkuu huyo wa Polisi aweze
kuhudhuria kikao kijacho(kesho) kwa ajili ya kupokea maoni na kujibu maswali ya
Madiwani kuhusu unyanyasi unaofanywa na Migambo kwa wananchi na boda boda.
No comments:
Post a Comment