Wanariadha wakipita katika moja ya barabara ya Arusha
wakichuana katika mbio za kilometa 10 wakati wa mashindano ya taifa ya wazi ya
Ngorongoro jana. (Na Mpigapicha Wetu).
Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 100 wakati
wa mashindano ya wazi ya taifa ya riadha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
jijini Arusha.
Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 5,000 za
wakati wa mashindano ya wazi ya taifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
Mwanariadha Fabiani Sule wa Jeshi la Polisi akimaliza namba moja katika mbio za mita 5000.
Wanariadha wa mbi za mita 5000 wakiwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Gidabuday akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Ramadhani Ng'anzi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MASHINDANO ya wazi ya taifa ya riadha yamefanyika
jijini Arusha na kushuhudiwa na watazamaji kibao waliofika kwenye Uwanja
wa Sheikh Amri Abeid.
Tofauti na mashindano hayo yanapofanyikia jijini Dar
es Salaam, uwanja huo ulikuwa na watazamaji kibao walioshuhudia wanariadha
wengi wa mkoa mwenyeji wakitamba katika mbio mbalimbali.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro kwa mara ya kwanza katika mashindano ya taifa yalishirikisha mbio
za barabarani za kilometa 10 badala ya zile za uwanjani za meta 10,000, ambazo jana hazikuwepo.
Katika mbio za kilometa 10, Jackson Mwakombe alimaliza
wa kwanza kwa kutumia dakika 32:00.22, baada ya kuongoza kwa muda mrefu mbio
hizo akiwaacha wenzake mbali.
Arusha pia ilitwaa medali ya dhahabu katika kilometa
10 kwa wanawake wakati Neema Kisuda alipomaliza wa kwanza kwa kutumia dakika 40:01.04
akifuatiwa na wanariadha wengine wa Arusha, ambao ni Gloria Makula na Sarah
Hiti waliomaliza katika nafasi ya pili na tatu kwa dakika 40:27.98 na 41:26.91.
Benjamin Michael alimaliza wa kwanza kwa kutumia
sekunde 10:99, huku Laurent Masatu na Bakari Barnabasi wote wa Arusha
wakimaliza katika nafsi ya pili na tatu kwa kutumia sekunde 11:10 na 11:18.
Katika mbio za meta 800, Mariam Salim, Grace Jackson
na Shamin Ramadhani wote wa Arusha walimaliza kwa dakika 2:18.09, 2:20.72 na
2:21.87 na kushika nafasi ya kwanza, ya pili na tatu kwenye Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid.
Kwa upande wa meta 5,000 wanawake, Arusha ilishika
nafasi mbili za kwanza pale, Natalia Elisante na Angelina Daniel walimaliza wa
kwanza kwa kutumia dakika 16:54.52 na 17:18.80 huku Angelina John wa Singida
akimaliza wa tatu kwa kutumia dakika 18:10.68.
Katika mbio za meta 800 kwa wanaume, mwanariadha wa
Manyara Gabriel Geay alitamba baada ya kumaliza wa kwanza kwa kutumia dakika
1:50.75 huku akifuatiwa na Faraja Damas na Simon Francis wote wa Arusha
waliotumia muda wa dakika 1:52.28 na 1:52.68.
Washindi wa kwanza katika kila mchezo wa mashindano
hayo yaliyodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, waliondoka na Sh
150,000 kila mmoja wakati wale walioshika nafasi za pili kila mmoja alipata
100,000 na watatu Sh 50,000.
No comments:
Post a Comment