KAMPENI ya 'Kila Mmoja
Anamfundisha Mmoja' (Each One Teach One) imeanzishwa na Mfuko wa UBA (UBA Foundation) ikilenga
kuwafanya wafanyakazi wa ALLUBA kupata fursa ya kurudisha kwa jamii walichonayo
kwa njia zao wenyewe.
Jitihada hizo zimelenga kuwasaidia vijana kupata ujuzi ambao
unaweza kuwasaidia kujitengeneza kipato (fedha) kwasiku za mbele.
UBA Tanzania kupitia Mfuko wa UBA imeshiriki katika kampeni ya
Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja kwa vijana wa Afrika.
Kupitia kampeni ya Kila Mmoja Anamfundisha Mmoja wafanyakazi wa UBA wanaojitolea wamekuwa
wakitumia muda wao kwenda katika jamii kufundisha vijana shughuli mbalimbali
kama vile lugha za kigeni, kupigapicha, kubuni mitindo, sanaa ya mapigano,
muziki na nyingine.
UBA si kwamba ina mtazamo wa kutoa mafunzo kwa vijana wa Dar
es Salaam na Dodoma tu, lakini ina mipango ya kuongeza programu katika maeneo
mengine ya nchi.
UBA imekuwepo nchini kwa miaka tisa sasa na imekuwa ikiitikia
vizuri wajibu wake kwa jamii.
No comments:
Post a Comment