HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 10, 2018

Taliss-IST yatwaa ubingwa wa kuogelea kwa waogeleaji chipukizi

Klabu nyota za mchezo wa kuogelea nchini, Taliss-IST, imetwaa ubingwa wa mashindano ya kuogelea kwa chipukizi kwa kuzishinda klabu nyingine saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mashindano hayo yaliyomalizika juzi kwenyebwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga. Taliss-IST imemaliza katika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake, Blueifins ambayo ni klabu changa, imemaliza katika nafasi ya pili kwa upande wa wanaume na wanawake hali kadhalika kwa kklabu ya DSC.

Taliss – IST ilipata pointi 1231.5 kwa upande wa wanaume na kufuatiwa na Bluefins iliyopata pointi 810.5 na DSC pointi 512 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya Pepsi.

Timu ya kuogelea kutoka mkoa wa Morogoro, Mis Piranhas ilishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 331 na kufuatiwa na Champion Rise (290), Wahoo ya Zanzibar (64) na Heaven of Peace Academy ilipata pointi 26.

Taliss-IST pia ilimaliza ya kwanza kwa upande wa wanawake, Taliss-IST ilipata pointi 1,595, Bluefins (686), DSC (619), Wahoo (251), Mis Piranhas (212), Heaven of Peace Academy( 8) na Champion Rise iliyopata pointi 4.

Mchezaji nyota wa timu hiyo, Aravind Raghavendran (12) alivuna pointi 220. Muogelaji huyo alitwaa medali 13 za dhahabu na kuweka rekodi mpya tisa katika mashindano hayo.

Pia muogeleaji nyota wa kike, Natalia Ladha aliweka rekodi mpya 11 na kutwaa medali za dhahabu 12 na mbili za shaba na kuwa mshindi wa Jumla katika kundi la waogealji wa kike wenye umri kati ya miaka 10 na 11. Sarah Imran Dewji ambaye alionyesha kuhimarika katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya waogeleaji 256 kutoka klabu mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alizipongeza klabu zote kwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo yaliwawezesha kupata waogeleaji chipukizi kadhaa kwa maendeleo ya mchezo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages