Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akisalimiana na ujumbe wa wafanyakazi Halotel ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung, ulipofika ofisini kwake kwa ajili ya kukabidhi msaada wa mashuka 150 na matanki ya kuhifadhia maji yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Januari 8, 2019. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akikagua sehemu ya msaada wa mashuka 150 yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya
Halotel kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za
kijamii.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, Januari 8, 2019.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashuka na matanki ya kuhifadhia maji kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, Januari 8, 2019.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada wa mashuka 150 pamoja na matanki ya kuhifadhia maji Januari 8, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada wa mashuka 150 pamoja na matanki ya kuhifadhia maji Januari 8, 2019.
Pokea shukrani zetu.....
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akipokea sehemu ya msaada wa mashukoa 150 kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Tien Dung (kushoto) kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akikagua matanki ya kuhifadhia maji yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Tien Dung.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akikagua matanki ya kuhifadhia maji yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Tien Dung.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akikagua matanki ya kuhifadhia maji yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Tien Dung.
Asanteni......
Tunashukuru..........
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, akimshukuru Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Tien Dung, baada ya kupokea msaada wa mashuka 150 pamoja na matanki ya kuhifadhia maji Januari 8, 2019.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA
kutekeleza mpango wake wa kurejesha faida kwa jamii na wateja kwa
ujumla, Kampuni ya Mawasiliano ya simu Halotel imetoa msaada wa matanki
kumi ya maji pamoja na mashuka 150 kwa Wilaya ya Kigamboni ili kusaidia
maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii.
Akizungumza
wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri
pamoja na kuipongeza Kampuni ya Halotel kwa msaada huo, pia alizitaka
taasisi zingine kuiga mfano huo utakaoisaidia wilaya hiyo na Serikali
kwa ujumla kupunguza changamoto zilizopo katika jamii.
Alisema
msaada huo umekuja wakati muafaka katika wilaya hiyo iliyoanzishwa hivi
karibuni kwa kuwa utawezesha maeneo yaliyokuwa na changamoto
mbalimbali yakiwemo ya Hospitali na shule kufikiwa na msaada huo na
hivyo kuondoa tatizo lilillokuwepo awali.
"Tunaipongeza
Halotel kwa kutenga sehemu yake ya faida na kuja kutoa msaada huu
katika wilaya yetu, msaada huu ni mkubwa kwetu na tunaamini kuwa
utatusaidia kutatua changamoto katika maeneo mbalimbali ya wilaya yetu
hususani wakati huu ambapo tunapambana kuboresha mazingira ya wilaya hii
changa" alisema Msafiri.
Aidha alisema Wilaya
ya Kigamboni bado ina mahitaji ya vitu mbalimbali wakati huu ambao bado
inazidi kukua ili iweze kutimiza malengo yake na kwamba ni wakati
muafaka kwa wadau wengine kujitokeza na kuisaidia ili iweze kutimiza
matakwa yake.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi
wa Halotel Nguyen Tien Dung, mbali na kuishukuru Serikali kwa kuweka
mazingira wezeshi kwa kampuni za simu kutoa huduma zake hapa nchini,
alisema uwepo wa kampuni hiyo hapa nchini umelenga kuhakikisha inawapa
wananchi wote huduma bora za mawasiliano,
Alisema
tangu kuingia kwake hapa nchini Halotel imekuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha inafikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi waliopo maeneo
mbalimbali ya nchi ikitoa huduma bora za mawasiliano pamoja na utumaji
wa fedha kupitia huduma ya Halopesa.
Naye Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda alisema,
msaada huo katika wilaya ya Kigamboni umelenga kuchangia maendeleo ya
wilaya hiyo.
Alisema kutokana na uchanga wa
wilaya hiyo, Halotel inaamini bado itakuwa inakabiliwa na changamoto
mbalimbali zikiwemo huduma za kijamii suala ambalo liliifanya kampuni
hiyo kuona kuwa ina kila sababu ya kuisaidia kwa lengo la kuunga mkono
juhudi za Serikali.
No comments:
Post a Comment