Mshindi wa
zawadi kubwa ya Sh. Mil. 50 katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo
Jigiftishe, Sadick Kilipamwambu (wa
tatu kushoto), akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini,
Abbas Abrahaman (wa pili kushoto). Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Tigo na
mshereheshaji wa shughuli hiyo Okechi Okechi. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Mkulima na mfanyabiashara wa
nyanya katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Sadick Kilipamwambu,
amejishindia kitita cha shilingi milioni 50 baada ya kuibuka mshindi katika
droo kubwa ya promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe.
Zabron ndiyo mshindi wa zawadi kubwa katika
Promosheni ya Jigiftishe. Washindi wengine katika droo kubwa ni Emma Kauka
mkazi wa Dar es Salaam na Abdulrazak Abdallah mkazi wa Zanzibar alijishindia Sh
15m/-.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhiwa
zawadi iliyofanyika katika Soko Manzese mjini Songea, Zabroni alisema maisha
yake yatabadilika kwa kiasi kikubwa kupitia fedha hizo.
“Sikuwahi kuwaza kumiliki kiasi kikubwa cha fedha
kama hiki…, maisha yangu yatabadilika. Nitajenga nyumba nzuri na kuachana na
kibanda cha nyasi nilichokuwa nikiishi na familia yangu. Naishuru Tigo kwa
kubadilisha maisha yangu,” alisema
Mshindi huyo alisema atatumia fedha hizo pia
kupanua shughuli zake za kilimo cha nyanya kwa kulima mashamba makubwa zaidi na
kwa klimo cha kisasa na pia atatumia fedha hizo kuwaendeleza watoto wake
kielimu.
Zabron alisema kushinda kwake
kunatokana na kuingiza vocha za Tigo kwa ajili ya kufanya mawasiliano na wateja
wake wa nyanya pamoja na kutuma au kutumiwa fedha mara kwa mara kupitia Tigo
–Pesa.
Akiongea wakati akimkabidi
zawadi kwa mshindi, Meneja wa Tigo kwa Kanda ya Kusini Abbas Abrahaman
aliwataka wakazi wa maeneo Songea na jirani kuendelea kutumia mtandao wa Tigo
ili kuweza kunufaika.
“Zipo faida nyingi za kutumia
Tigo. Ni mtandao wa uhakika na gharama nafuu. Leo mmeshuhudia mwenzenu akiweza
kujishindia Sh milioni 50m/-kwa kutumia tu mtandao wa Tigo na hii inaonyesha
kuwa Tigo inawajaili wateja wake,”alisema.
No comments:
Post a Comment