HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 10, 2019

TAMWA YAPONGEZWA ZANZIBAR

Mauwa Mussa, Zanzibar

Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya shehia ya Umbuji wilaya ya kati Unguja, wamekipongeza chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA - Zanzibar kwa kujitolea kuwapa elimu juu ya kupigania haki zao za msingi.

Waliyaeleza hayo  walipokua wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa lengo la kutaka kujua ni kwa namna gani wananchi wamehamasika kuzungumzia mambo mbalimbali katika jamii zao ikiwamo changamoto tofauti zinazowakabili.

Mmoja kati ya wanakijiji hao aliyejitambulisha kwa jina la Patima Vuaa Hassan alisema, TAMWA walifika kijijini kwao na kuwapa elimu ya kujitambua katika hazi zao za msingi kama vile huduma ya kupata afya, maji na nyenginezo.

Alisema hivi sasa wameshaanza kupigia mbio kituo cha afya kwani kilichopo kimekuwa ni chakavu  na haduma haziendi vizuri kama inavyotakiwa.

“ukweli tulikaa tukasikitika sana kwa sababu kituo ni kidogo,  tunawataka watujengee bandaa ili watu waenee” alisema mwananchi huyo.

Haji Shauri Issa alisema, anatamani kuona mradi wa PAZA haumaliziki, kwa sababu umewafunza mambo tofauti.

“kwanza umetufunza , kujua taratibu za wapi tunaweza kupeleka malalamiko yetu, yaani hatua za awali za kufuatilia jambo mfano katika jengo la skuli na tupo katika hatua nzuri” alisema Issa.

Shauri aliendelea kueleza, wameshaanza kufuatilia changamoto zilizopo katika kituo cha afya na anamini watafanikiwa.

Daktari dhamana wilaya ya kati Tatu Ali Amour alisema, wamepokea vilio vya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo watu wa Umbuji juu ya changamoto katika kituo chao cha afya.

Dk Tatu alisema, changamoto hizo wameshazisikia na baadhi yao wamesha zitatua na hatua mbalimbali zinaendelea kuweka mazingira mazuri.

Akizungumzia maendeleo ya wananchi alisema , awali  walikua na dhana yakua dawa hakuna tu na walikua wakilalamika sana, lakini walipoamua kutaka kujua kiundani waliwaeleza kwamba kuna aina ya dawa huja kwa awamu au kipindi maalum, hivyo walifahamu na hivi sasa malalamiko hayo yamepungua.

“mradi ndio uliyosaidia, mana walitaka kujua kwakina, tofauti na hali ilivyokua awali, tunahitaji mradi uendelee”alisema daktari huyo.

Mradi wa PAZA ulianza Novemba 2017 na unatarajiwa kumalizika Febuari 2019 mradi ambao unatekelezwa katika wilaya tatu za nguja (wilaya ya kaskazini A, wilaya ya kati na wilaya ya kusini ) na Pemba pia upo katika wilaya tatu ( Wilaya ya chakechake, wilaya ya Wete na wilaya na Micheweni)


Mradi unasimamiwa na kutekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzaniab-Zanzibar – TAMWA, Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar – WAHAMAZA pamoja na NGENAREKO kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

Pages