Shirikisho la Riadha Tanzania linapenda kurudia kwa
msisitizo utaratibu wa namna ya kuendesha mashindano ya mbio za barabarani ikiwemo
marathon (42k).
Mwaka jana tumeshuhudia utaratibu holela kiasi kwamba watu
wanaandaa mambo yao bila hata kuomba utaratibu kwa RT kitu ambacho ni
kinyume cha sheria za Baraza la Michezo la Taifa.
Nawataarifu wote wenye nia njema ya kuandaa mashindano
waelekeze maombi yao ofisi kuu ya RT iliyopo Taifa Road Temeke Dar es
Salaam (inatazamana na uwanja wa taifa).
Kinyume na hapo tutawasiliana na sponsors wote kuwataarifu
kwamba RT haitatambua mchango wa udhamini wowote kwenye mbio ambazo
Shirikisho haijashirikishwa, hivyo ni vyema sponsors wote wawasiliane na
RT kabla ya kuingia makubaliano na waandaaji wa mbio husika.
Pia RT inayo uwezo wa kuwazuia wanariadha wake kushiriki mbio zozote haramu (kama RT haijahusishwa).
Kwa mbio ambazo ni chini ya kilomita 21 hakuna Ada ila ni
lazima RT ikatoa baraka zake kwa wahusika kulipa Ada ya usajili
(registration fee) ambayo ni 100,000 tu na inalipwa mara moja kwa uhai
wa mbio zenyewe.
Nimekusudia kutoa tamko hili kutokana na ukweli kwamba kuna
ukanjanja katika kuandaa mashindano haya, nawasihi waandaaji wote waige
mfano wa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon, Tulia Marathon, Rock City
Marathon nk.
Wilhelm Gidabuday
Katibu Mkuu-RT
No comments:
Post a Comment