Mwakilishi wa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw.Ilusubisya Kasebele akizungumza na wadau wa Ustawi wa Jamii jijini
Dodoma wakati akifungua kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa utoaji
huduma kwa wahanga wa ukatili katika Mpango
Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema mapema mwezi huu itazindua mkakati wa
Kitaifa wa kutokomeza mauji dhidi ya wazee ikiwa ni jitihada za kupambana na ukatili kwa wazee nchini kwani
nguvu kubwa imeelekezwa katika ukatili kwa wanawake na watoto.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Afisa
Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Amina Mafita wakati akizungumza
katika kikao kilichokutanisha wadau wa ustawi wa Jamii kilichokutana
kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya
Wanawake na Watoto hasa katika utoaji wa huduma kwa wahanaga wa vitendo hivyo.
Bi. Amina ameeleza kuwa Mpango Mkakati huo wa
Kutokomeza Mauaji ya Wazee utasaidia kuinua hari ya wadau katika kuweka nguvu
na kutoa elimu kwa jamii kupambana na mauji hayo mabayo mengi yamekuwa
yakihusishwa na imani za kishirikiana
katika baadhi ya maeneo nchini.
Ameongeza kuwa Mkakati huo umeshakamilika na upo
tayari na utazinduliwa hivi karibuni ili kuwezesha kutokomeza mauji ya wazee na
Mkakati huo ni sehemu yautekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili
dhidi ya wanawake na watoto nchini.
“Sasa tumeamua kuangalia na upande wa Wazee kwani
nao wanafanyiwa vitendo vya ukatili hasa kuuwawa kikatili katika maeneo mbalimbali nchini” alisisitiza
Bi. Amina.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bw.
Darius Damas amesema kuwa Serikali inaendelea
kushirikiana na wadau katika kuendelea na kupambana na ukatili wa Kijinsia
kwani ni watu muhimu katika mapambano hayo.
Amesisitiza kuwa katika Mpango Mkakati wa Kutokomeza
Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto wadau hao wanakutana kwa lengo maususi la
kueleza utekelezaji wa wadau katika utoaji wa huduma kwa wahanga wa vitendo ya
ukatili.
Ameongeza kuwa katika kuwezesha utoaji wa huduma
kwa wahanga wa vitendo ya ukatili nchini kuna umuhimu wa uwepo wa nyumba salama
kwani wengi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ni wanawake na watoto na inasaidia
sana kutunza ushaidi wa kesi za ukatili ili kuendelea na kupambana na Vitendo ya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto nchini.
Naye Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mtaifa
linaloshughulikia Wahamiaji (IMO) Bi. Inna Lutengano amesema kuwa Shirika lake linashirkiana na
Serikali na Mashirika mengine kutoa
elimu kwa jamii kuhusu masuala ya usafrishaji haramu wa binadamu ambapo vitendo
hivyo huendana na vitendo vya ukatili na uathiri sana wanawake na watoto.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Railway
Children Africa Bi. Mary Katama amesema kuwa Shirika lao limejikita katika
kuwasaidia watoto wa mitaani na wengi wao wakiwa wamekimbia sehemu wanazoishi
kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
Ameeleza kuwa wamekuwa wakitoa nafunzo kwa watoto na
wazazi kuhusu malezi bora na kuhakikisha kuna usalama katika familia ndipo
huwarudisha watoto hao katika familia zao na kwa wale walio na umri kuanzia miaka
15 wanawapatiwa stadi za kazi ili kujiendeleza na kujitegemea.
Kikosi kazi cha utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWA) kwa upande wa utoaji
wa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
kiekutana jiji ni Dodoma ikiwa ni miongoni mwa vikao vya kila mara
wanavyokutana kupeana mrejesho wa utekelzaji wa majukumu yake.
No comments:
Post a Comment