Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa
Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako
aliongoza kikao cha wadau wa zao la korosho, Januari 27, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa kIkao cha wadau wa zao la korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika kikao hicho alichokiitisha mjini Mtwara, Januari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao alichokiitisha cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika mjini Mtwara, Januari 27, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Februari 5 wawe wamekamilisha uhakiki na malipo kwa wakulima wa korosho

WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya
Mazao Mchanganyiko wahakikishe hadi Februari 5 mwaka huu wawe
wamekamilisha uhakiki na kuwalipa wakulima wote wa zao la korosho.
Pia
amesema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa mazao makuu ya
biashara kuanzia hatua ya uzalishaji hadi masoko yake likiwemo zao la
korosho kwa lengo la kuwapatia tija wakulima.
Amesema
zao la korosho ambalo awali soko lake halikwenda vizuri kutokana na
utaratibu uliokuwa ukitumiwa na wafanyabiashara kwa kutenda bei ndogo na
wakulima wenyewe kugomea bei hiyo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Januari 27, 2019) wakati akizungumza
na wadau wa zao la korosho mkoani Mtwara, lengo likiwa ni kupata
taarifa juu ya mwenendo mzima wa bidhaa hiyo kwa msimu wa mwaka
2018/2019.
Amesema
Serikali ilitoa nafasi kwa wafanyabishara kufanya marekebisho ili
waweze kununua bidhaa hiyo kwa bei nzuri bila mafanikia hali
iliyopelekea Serikali kuamua kununua korosho zote ili wakulima wapate
tija.
Naibu
Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa, taarifa iliyotolewa na timu
ya uhakiki ilisema msimu wa 2018/2019 matarajia yalikuwa ni kuvuna tani
150,000 kutokana na kushuka kwa uzalishali.
“Lakini
kwa kazi nzuri iliyofanywa na timu nzima ya Wizara, wilaya na mkoa na
timu ya uhakiki hadi sasa korosho tulizozipokea ambazo ziko katika
maghala ni zaidi ya tani laki mbili.”
Amesema
zoezi hilo limewapa tija kubwa katika zao hilo tofauti na taarifa
zilizowafikia hapo awali, ambapo wanatarajia baada ya zoezi hilo
kumalizika watafikisha zaidi ya tani 200,000 ikiwa ni nyongeza zaidi ya
tani 100,000.
Amesema,
Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa hapa nchini ni Tandahimba
amabpo wamefikia asilimia 96 ya uhakiki hadi kufikia jana huku zoezi la
malipo kwa korosho zote zilizohakikiwa kwa mkoa wa Mtwara yamefikia
asilimia 83.
Hata
hivyo, Waziri huyo amesema kuwa fedha za kununulia korosho hizo zipo
kwa kuwa Serikali imejipanga vizuri. Jumla ya sh bilioni 700 zimetengwa
kwa ajili ya zoezi hilo ambapo hadi sasa zaidi ya sh. bilioni 400
zimeshalipwa wakulima waliohakikiwa hadi juzi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,
JUMAPILI, JANUARI 27, 2019.
No comments:
Post a Comment