Wanafunzi wa Shule ya sekondari Mtitaa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wakiwa kwenye madawati muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Benki ya NMB jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Mwanahamisi Mkunda (kushoto), akipeana mkono na Meneja wa Benki NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi, ikiwa ni ishira ya kukabidhiwa viti na meza 50 pamoja na viti 71 vya maabara kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mtitaa na Bahi, makabidhiano hayo yalifanyika shule ya sekondari Mtitaa jana. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
WAZAZI
na walezi wilyanai Bahi mkoani Dodoma, wametakiwa kuunga mkono juhudi
za Serikali ya awamu tano chini ya Rais John Magufuli kwa kuchangia
vifaa vya shule ili kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya elimu
nchini.
Hayo
yamelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi (DC), Mwanahamisi Mkunda, wakati
alipozungumza kwenye makabidhiano ya msaada wa viti na meza kutoka Benki
ya NMB, yaliyofanyika katika viunga vya Shule ya Sekondari ya Mtitaa,
Wilayani Bahi.
DC
Mkunda aliwataka wazazi na walezi kupambana kadri wawezavyo kuhakikisha
wanaisaidia Serikali kuchangia baadhi ya vifaa vya elimu ili kupunguza
changamoto ya vifaa hivyo.
“Mkiaambiwa
elimu bure, msifikiri kila kitu ni bure kuna baadhi ya vifaa wazazi
mnatakiwa kuchangia, haiwezekani hata dawati Serikali ifanye pekee
yake,” alisema.
Mkunda
alivitaja baadhi ya vifaa vya elimu wanavyotakiwa kuchangia wanachi na
jamii kwa ujumla kuwa ni madawati, vitabu, madaftari na vingine ambavyo
vinatumika katika kutoa elimu, ambalo ni jukumu lao kujitolea.
Aidha
alitoa muda wa miezi mitatu kwa wakazi wa Kata ya Mtitaa wilayani
haumo kuhakikisha wanamaliza changamoto ya viti na meza vilivyobaki.
Naye
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mtitaa, Selemani Mbiaji, aliishukuru
Benki ya NMB kwa msaada waliotoa kwa ajili ya shule hiyo na kuahidi
kuvitunza vifaa hivyo.
Mbiaji
alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 332 na idadi ya viti na meza
vilivyopo ni 201, hivyo baada ya msaada huo kutoka NMB, wataendelea kuwa
na upungufu wa viti 131.
Kwa
upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi, alisema msaada
huo waliokabidhi una thamani ya Shilingi milioni 10, huku akivitaja
vifaa walivyokabidhi kwa shule mbili za Sekondari za Mtitaa na Bahi,
kuwa ni viti na meza 51 na viti maalumu 71 vya kutumika kwenye maabara.
Mlozi
alisema lengo la NMB hiyo kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhusi za
Serikali ya awamu ya tano katika kuhudumia jamii kwa kutenga asilimia
moja ya faida inayopata kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment