HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 14, 2019

BENKI YA CRDB YAKWANZA KUUZA FEDHA ZA KIGENI ARUSHA

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati wakiingia ukumbini kwa ajili ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wafanyabiashara na wateja wa benki hiyo, iliyofanyika kwenye jijini Arusha leo. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, wakati wa uzinduzi wa semina kwa wafanyabiasha na wateja wa benki hiyo jijini Arusha.
 Picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, wakati wa uzinduzi wa semina kwa wafanyabiasha na wateja wa benki hiyo jijini Arusha.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay.

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameimwagia sifa Benki ya CRDB kwa kuwa ya kwanza kufanyabiashara ya ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni baada ya serikali kufungia baadhi ya maduka ya biashara hiyo jijini Arusha. 
Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini hapa, Gambo alisema ubunifu na uharaka waliouonyesha watendaji wa CRDB kwenye biashara hiyo unaakisi juhudi za serikali za kujenga uchumi endelevu na wenye kugusa sekta zote za uzalishaji.
“Kama mtakumbuka, serikali iliamua kuingilia kati suala la maduka ya kubadilishia fedha nchini, hususani hapa Arusha ili kubaini maduka yanayofanya biashara hizo kinyume cha sheria na taratibu. Zoezi hilo lilisababisha kufungwa kwa baadhi ya maduka na kuleta upungufu wa huduma za fedha za kigeni. 
“…Kitendo chenu cha kuweka dirisha maalum kwenye matawi yenu yote ili yatoe huduma za uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni, umeonyesha kwa kiasi gani nyinyi ni wazelendo wenye nia njema ya kuona juhudi za serikali ya awamu ya tano, hongereni sana,” alisema Gumbo.
Alitumia fursa hiyo kuitaka CRDB kuangalia jinsi ya kuboresha huduma hiyo kwa kuongeza muda wa kutoa huduma katika matawi yake kwa kuwa watalii wengi huhitaji huduma ya kubadilisha fedha kwa muda ambao matawi ya benki yamefungwa. 
Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki hiyo imejipanga vizuri kutoa huduma stahiki kwa wakazi wa Arusha na nchi nzima.
“Nichukue fursa hii kuwahakikishia wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa matawi yetu saba yapo tayari kuwahudumia. Huduma zetu zina kidhi mahitaji ya makundi yote ya jamii kuanzia watoto, wakubwa, kinamama, wafanyabishara wadogo, wakati na wakubwa. 
“Pia tunafanya biashara za Bima na kukusanya malipo yote ya serikali kuanzia ankara, kodi na mengineyo. Pia Benki inawahudumia wateja wadogowadogo kupitia  kitengo chake cha wajasiliamari yaani CRDB Bank Microfinace,” alisema  Nsekela.
Semina ya hiyo ni sehemu ya mipango mkakati wake wa kuwafikia wateja wake ili kuwaainishia huduma zinazopatikana ndani ya CRDB zitakazowanufaisha kibiashara huku ikikusanya maoni yao juu ya njia bora zaidi za kuwahudumia

No comments:

Post a Comment

Pages