Mkurugenzi Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Tausi Mwilima (kulia) kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, akielezea faida za NGOs kusajili ndani ya Sheria ya NGO Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 wakati wa kikao cha wadau wa Mashirika hayo kilichofanyika Mkoani Kilimajaro, wengine ni Msajili wa NGOs Bi. Neema Mwanga (wa tatu kushoto), akifuatiwa na Katibu Tawala Msaidizi– Mipango Bi. Lydia Liwa (wa pili kushoto) na (Kushoto) ni Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro B. Hilda Lauwo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Vyanzo
vya mapato ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali sio siri kwa kuwa fedha hizo zitafutwa kwa
kutumia majina na taarifa za wanajamii hao hivyo fedha za mradi zinapoatikana isiwe
siri katika utumikaji wake.
Hayo
yamesemwa na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya-
Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto B. Neema Mwanga
alipofanya kikao na wadau wa Mashirika ya NGOs wanaofanya kazi zao katika wilaya
zote za Mkoa wa Kilimanjaro.
Bi Mwanga amewaagiza wamiliki wa Mashirika hayo
kote nchini kuhakikisha kuwa taarifa za vyanzo vya fedha vinakuwa wazi ili
wanajamii waweze kuzifahamu na kutumika kwa mujibu wa andiko la maombi ya
rasilimali hizo.
“Vyanzo
vya mapato ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali sio jambo la siri, tunapoandaa maandiko
ya miradi yetu tunatumia taarifa za majina ya wananchi walioathirika katika maeneo
husika hivyo Mashirika hayo kuficha taarifa za fedha hii sio haki”. Alisema.
Msajili
ameongeza kuwa kila Shirika Lisilo la Kiserikali sharti liwe na Sera ya
uendeshaji wa Shirika husika na Kanuni za maadili pamoja na Sera ya kuzuia
kushwa mahala pa ili kuhakikisha kuwa Shirika linalinda maslahi ya taifa na
kukuza haki na utu wa wanajamii
wanaonufaika na miradi inayotekelezwa.
Msajili huyo ameelekeza uongozi wa Mashirika hayo kuhakikisha yanafanya tafiti
ili kujua na tathmini ya matatizo ya kijamii kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa Serikali kabla ya kuomba fedha kutoka kwa wahisani kwa lengo la
kutekeleza miradi inayozingatia vipaumbele vya kitaifa na mahitaji ya makundi
mbalimbali katika jamii zetu.
Ameongeza kuwa Mashirika hayo yanaowajibu wa kuwa na daftari la mali za shirika ambazo
zimenunuliwa na kulitunza ipasavyo na daftari hilo litaboreshwa kila mara ili
kuhakikisha kuwa mali zote za Shirika zinahuishwa ili kukuza udhibiti
wa mali hizo.
Aidha,
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ametoa agizo kwa wadau wa NGOs
kuhakikisha wanawasilisha taarifa za mwaka na kulipa ada kwa wakati.
Aidha ameongeza
kuwa taarifa za fedha zitakazowasilishwa ziwe zimekaguliwa ili kutoa taswira
ya halisi ya mapato ya Shirika kulingana na miradi iliyopokea fedha.
No comments:
Post a Comment