HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2019

UTT AMIS YAWANOA WASTAAFU MKOANI MOROGORO

UTT AMIS ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Fedha ambayo inatoa huduma ya Uwekezaji kupitia mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.

Kwa sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu na Ukwasi.

UTT AMIS hutoa elimu bure kwa makundi mbalimbali ili kuwawezesha kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji.

Kwa sasa timu ya maafisa wa UTT AMIS walishiriki katika mafunzo ya wastaafu yaliyoandaliwa na Kampuni ya Taifa ya Tija ya (NIP) ili kuwajengea wastaafu watarajiwa uelewa mpana juu ya mpango wa uwekezaji kwenye mifuko inayoendeshwa na UTT.
 
Baadhi ya washiriki wa semina ya wastaafu iliyoandaliwa na Shirika la Tija la Taifa 'National Institute of Productivity' wakisikiliza mada juu ya uwekezaji wa pamoja pindi watakapostaafu.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wastaafu mkoani Morogoro iliyoandaliwa na Shirika la Tija la Taifa 'National Institute of Productivity'.
 Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku, akisikiliza maswali kutoka kwa washiriki wa semina.

No comments:

Post a Comment

Pages