NA TIGANYA VINCENT, TABORA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewaaziga viongozi mkoani Tabora kuhakikisha watoa elimu kwa wananchi ili wengi wajiunge na Bima ya Afya.
Hatua hiyo inalenga kuwafanya wananchi itakayowawezesha kupata huduma mwaka mzima bila kuwa na mashaka.
Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali za maendeleo katika Halmashauri ya Mji Nzega mkoani Tabora.
Alisema kuwa sio kila wakati mwananchi atakuwa na fedha kwa ajili ya kugharimia matatibu yake ni vema akawa na Bima ili kupata uhakika wa afya yake.
Makamu wa Rais alisema kwa kulitambua hilo inakusudia kupeleka Bungeni muswada wa wa Bima ya Afya ambayo kila mwananchi atatakiwa kujiunga ili kuwa na uhakika wa matibabu mwaka mzima.
“Sio wakati wote mtakuwa na fedha kwa ajili ya kugharimia matibabu yenu …jiungeni na bima ya afya ili muwe na uhakika wa kulinda afaya zenu mwaka mzima”alisisitiza.
Alisema Serikali itaendelea kuboresha miundo mbinu na upatikanaji wa vifaa tiba na wataalamu ili kuhakikisha huduma zote zinapatikana kwa wananchi.
Kwa upande wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwita Waitara aliwataka wasimamizi wote wa ujenzi wa vituo vya afya nchini kuhakikisha wanazingatia ramani za ujenzi walizopewa na TAMISEMI ambazo zinawataka kujenga majengo matano
No comments:
Post a Comment