Adam
Ahmed
Natalia Ladha
Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST
yamepangwa kufanyika kwenye bwawa la
kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga kwa siku mbili
kuanzia Februari 9.
Mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji wenye umri tofauti
kwa mujibu wa meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe.
Hadija alisema kuwa wanatarajia kupata ushindani mkubwa
katika mashindano hayo ambayo yameandaliwa kwa ajili kupima maendeleo na uwezo
wa waogeleaji baada ya kufanya mazoezi.
Alisema kuwa klabu yao imejipanga kuendesha mashindano yenye
ushidani mkubwa chini ya usimamizi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA).
Alifafanua kwa wanatarajia kupata waogeleaji kutoka mikoa
mbalimbali ikiwa pamoja na Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam
na Zanzibar.
“Haya mashindano ya kupima maendeleo ya waogeaji wenye umri
tofauti na maandalizi yake yamekwisha kamilika. Waogeleaji watashindana katika
staili tano tofauti na vile vile kushindana kwenye ‘relay’,” alisema Hadija.
Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya
waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa
kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.
Staili ambazo waogeleaji watashindania ni Backstroke, Butterfly,
Freestyle, Breaststroke na Individual Medley (IM).
Waogeleaji watakuwa katika makundi ya umri tofauti ikiwa
pamoja na chini ya miaka nane (8), 9 na 10, 11 na 12, 13 na 14 na wenye miaka
kuanzia 15 na zaidi.
Washindi kwa upande wa wanawake na wanaume watazwadiwa
medali ikiwa pamoja na dhahabu, fedha na shaba wakati washindi wa kwanza, kwa
makundi ya umri watazawadiwa vikombe.
No comments:
Post a Comment