Kikundi cha Mwiduka kutoka Mkoani Mbeya kikitoa burudani katika mkutano wa utambulisho kwa vyombo vya Habari, Zanzibar.
NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR
WAFANYABIASHARA na wananchi wote wa Zanzibar, wametakiwa
kuwa kifua mbele kila msimu wa uwepo wa tamasha kubwa la Kimataifa la muziki la
Sauti za Busara kwa kuwa tamasha hilo linabeba taswira chanya ya maendeleo ya
Wanzibar wote.
Ambapo pia amewataka kuchangamkia fursa ya uwepo wake kila
mwaka kwani limekuwa likileta wageni wengi
wanaokuja nchini kuhudhuria tukio hilo kubwa lenye kuvutia watu
mbalimbali Duniani kote.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini
hapa, Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed Said, amesema tamasha
hilo la siku nne ni kichocheo cha uchumi kwani watu wanafika mbali na
kulishuhudia lakini pia wanafanya manunuzi na matumizi ndani ya Visiwa hivyo na
kuongeza pato la Serikali.
“Kuanzia leo tutashudia burudani ya muziki kutoka kwa wasanii
mbalimbali wa ndani na nje, wanamuziki hao wataonesha nyimbo za tamaduni za Nchi zao huku pamoja na kutoa burudani na
mafunzo kwa watu wote.
Muziki ni biashara, muziki ni kazi na ni kazi kubwa hivyo
ili kuwaunga mkono wasanii hawa ni kujitokeza kushuhudia tamasha hili ambapo
pia tumetoa ofa ya punguzo kubwa kwa wenyeji.” Alisema Simai.
Aidha, Simai alisema viongozi wa Busara Promotions ambao ni waasisi na waandaaji wa tamasha hilo,
wamekuwa wakifanya kila aina ya mbinu kuhakikisha linaandaliwa na kufanyika kwa
ubora uliokusudiwa hivyo ni juu ya wananchi haswa wazanzibar kulikubali na kulithamini ili
kuinua hadhi ya Zanzibar kimataifa.
“Ili tamasha ni la kwenu Wazanzibar. Tuliinue tulipendemilango
ipo wazi kwa wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kulidhamini kwa aina yoyote
ile ya udhamini utapokelewa. Tunahitaji liweze kuwa thamani zaidi na tulienzi kwa kiwango cha juu”
alisema Simai ambapo amesisitiza kuwa uwepo wa tamasha hilo si kwa ajili ya
kuvutia watalii pekee bali kwa watu wote kwenye nyanja za Utamaduni, mila na
desturi za mwafrika kupitia njia ya muziki.
Simai pia amesisitiza kwa
vyombo vya habari na wataalamu wa teknolojia ya habari Nchini kuendelea
kuwaunga mkono katika kutangaza taarifa za habari za tamasha hilo ikiwemo mandhari
ya mji wa Zanzibar ili lionekane duniani kote na kuwatia hamu wale ambao
hawajawahi kufika Zanzibar kuamua kwenda kushuhudia.
Kwa upande wao Mabalozi wa Uswis na Norway wanaoziwakilisha nchini
zao hapa Tanzania, wamewapongeza Busara Promotions kwa namna wanavyoendesha
tamasha hilo ikiwemo kukuza tamaduni za Mwafrika kupitia njia za Sanaa.
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Bi. Tinguely Mattli amesema
wanaamini tamasha hilo ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kupitia
wasanii ambao wamekuwa ni kioo cha jamii.
Nae Mwakilishi wa Balozi wa
Norway nchini na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano, Trygve Bendiksby alisema
kupitia kauli mbiu ya mapambano dhdi ya rushwa ujumbe utafika kwa wakati na
haraka kupitia wasanii ambao jamii imekuwa ikiwafuatilia kwa ukaribu hivyo
wataendelea kudhamini tamasha hilo kwa kipindi kingine.
“Tunaungana na Busara Promotions kwenye tamasha ili kubwa na
tutaendelea kulidhamini tamasha kwa kipindi kipindi cha miaka mitatu mingine”
alisema Bendiksby.
Ubalozi huo wa Norway na Busara Promotions wanatarajia
kutiliana saini ya udhamini wa miaka mitatu mingine hapo baadae. Tayari Norway
imeweza kulidhamini tamasha hilo kwa muda wa miaka tisa (9) kwa kipindi
tofautitofauti.
Naye Mkurugenzi wa Busara Promotions, Mahmoud Yusuf amesema
kuwa, wamekuwa wakipokea maombi mengi ya
wasanii ndani na nje ambapo walio na sifa ndio wenye kuchaguliwa
kila mwaka ambapo kwa mwaka huu karibu wote waliochaguliwa ni wa kiwango cha
juu.
“Watu ni wengi na karibu hoteli zote zenye hadhi ya nyota
nne na tano hususan maeneo ya Mji Mkongwe zimejaa na maeneo mengine watu
wamejiandaa kwa ajili ya tamasha ili kubwa visiwani hapa” alisema Yusuf.
Yusuf amesema kuwa, wenyeji wamepewa nafasi ya kipekee ya
kushuhudia tamasha hilo kwa bei ya ofa maalum kwa siku tsh. 10,000 huku kwa
siku zote nne akitakiwa kulipa tsh. 20,000 huku akitaka pia wawe mfano wa
kuigwa kwa kuonesha ukarimu na upendo kwa wageni kuanzia vyombo vya usafiri
maeneo ya mitaa na manunuzi ili wajisikie wapo na wenyeji wenye moyo wa kupokea
wageni.
Naye Meneja waTamasha hilo, Ramadhan Journey alisema kuwa, kwa mwaka huu ni la 16 vikundi 44,
vinatarajia kuonesha burudani kwa siku
nne kwenye majukwaa matatu tofauti ya katika ukumbi wa kihistoria wa ‘Old Fort’
mjini Stone Town, Zanzibar.
Aidha, Journey ametaja baadhi ya orodha ya Wasanii kwa mwaka
huu ni akiwemo: Fid Q kutoka Tanzania
Bara, Wasanii wengine na Nchi zao kwenye mabano
ni pamoja na: Mokoomba (Zimbabwe), Afrigo Band (Uganda), Fadhilee Itulya
(Kenya), Ifrikya Spirit (Algeria), Rajab Suleiman & Kithara ( Zanzibar),
Tune Recreation Committee, (Afrika Kusini), Ithrene (Algeria). Hoba Hoba Spirit
(Morocco).
Pia wamo: M'Toro Chamou (Mayotte/Reunion), Trio Kazanchis +2
(Ethiopia/Switzerland), Faith Mussa (Malawi), Shamsi Music (Kenya), Sofaz (Reunion), Dago Roots( Reunion), Lydol (Cameroun), Jackie Akello (Uganda), S Kide
& Wakupeti Band (Tanzania), Tausi Women's Taarab (Zanzibar), Mkubwa na
Wanawe Crew (Tanzania), Damian Soul (Tanzania) na Wamwiduka Band (Tanzania) na wengineo.
No comments:
Post a Comment