Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita, Meja Jenerali Alfred Kapinga (katikati), akizungumza na wakuu wa shule zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ (hawako pichani) katika kikao cha Utendaji kuhusu maboresho ya shule hizo jijini Dar es Salaaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
Wakuu wa Shule zinazomilikiwa na jeshi la ulinzi la
wananchi JWTZ wametakiwa kuboresha uendeshaji
wa shule hizo ili kuendana na kasi ya Serikali na kukidhi mahitaji na mwongozo wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Magufuli kuwa nchi ya uchumi wa kati
kwa kuzalisha wahitimu wanaoendana na azimio hilo.
Maagizo hayo yalitolewa na Mkuu wa mafunzo na
Utendaji Kivita JWTZ Meja Jenerali
Alfred Kapinga wakati wa Kikao na Wakuu hao wa Shule yenye lengo la kutathmini
na kuweka maazimio kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi Jijini Dar es
Salaam.
Alisema kufanya vizuri kwa shule za Jeshi ni wajibu
ambao pia umekuwa ukisisistizwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance
mabeyo kutokana na mazingira ya Shule husika.
“ Hatuna sababu kuacha kujitofautisha na shule za kiraia kutokana na
mazingira ya shule zetu ziliko na Walimu katika shule hizo wakiwemo ambao ni wanajeshi
hivyo ni matarajio ya Mkuu wa Majeshi kuona Utofauti huo kutokana na wananfunzi
wanaohitimu katika shule hizo.” Alisema Meja jenerali Kapinga.
Aliongeza kuwa mwanafunzi anayemaliza katika Shule
ya jeshi la Anga Ngerengere na Anayemaliza katika Shule ya Wanamaji Kigamboni
na anayemaliza Makongo na shule nyingine Wanatakiwa kuwa tofauti kutokana na
Elimu ya Ziada iliyotokana na Fursa ya Uwepo wa shule katika mazingira husika.
Pia aliwataka Kuanzisha Mafunzo ya Ufundi Stadi ili
nayo kuwa Sehemu ya Utofauti wa Shule hizo kwa kuzalisha Wataalamu wa kati na
wa chini watakaojiajiri lakini pia kuajiriwa katika Viwanda na fani husika.
“ Navy
niliwaelekeza wameanza na wameanza kwa mafanikio sasa kilichobaki ni
kuboresha elimu inayotolewa na chuo ili
kuweza pia kujitangaza na kuwa fursa ya kupata Wanafunzi wa Kutosha na kutoa Mchango stahili kwa Nchi”. Alisema Mkuu huyo wa Mafunzo na utendaji
Kivita.
Aliongeza
kuwa nidhamu ni kitu muhimu hivyo wanafunzi wanaomaliza katika Shule za kijeshi
wanatakiwa kuwa na nidhamu zaidi kuliko wanafunzi katika shule nyingine
wakiakisi Nidhamu iliyoko katika jeshi ingawa yasiwe mafunzo kama ilivyokuwa
kwa Shule ya Wavulana ya Tabora.
Wakuu hao wa shule za JWTZ wameahidi kufanyia kazi
maazimio hayo ikiwa pia ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo kurejesha majina ya shule za jeshi ikiwemo uanzishaji wa vyuo vya ufundi kwa
fani zilizokaribu na shule husika
Miongoni mwa maazimio walioweka ni uanzisjhaji
masomo ya Sayansi ya Kijeshi, kusimamia ipasavyo walimu,nidhamu, uboreshaji
miundombinu uanzishwaji klabu za hesabu,kufufua vipaji kwa shule za michezo na kuboresha
mahusiano na wadau wengine wa elimu ili kuendana na mabadiliko.
Pia Wakuu hao
wa Shule wameazimia Kuongeza Ufaulu kwa kuondoa
Divisheni O kwa baadhi ya Shule zilizopata matokeo hayo na Divisheni IV kwa shule zenye ufaulu wa mwisho wa Divisheni
IV kwa wahitimu wa Kidato cha Nne na
Sita na Ufaulu wa chini kubakia Divisheni III.
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania linamiliki
Shule 10 Nchini ambazo ni Nyuki Unguja ,
Al Khamis Camp Pemba, Airwing, Makongo Jitegemee na Kigambo zilizoko Dar es salaam, Ruhuwiko
Songea,Unyanyembe Tabora, Kawawa Mafinga Iringa
na Kizuka Morogoro.
Uanzishwaji wa shule hizo ulikuwa na Lengo la kutoa Elimu kwa Askari wake na
baadae kutoa Elimu kwa Familia za Askari husika lakini baadae kwa jamii Nzima
ambayo imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na Shule hizo
No comments:
Post a Comment