Na Talib Ussi
Wizara ya Afya Zanzibar imesema Vifo vya akina mama na watoto wachanga katika Visiwa
vya Zanzibar vimepungua kutoka vifo 237 hadi kufikia 219 kwa mwaka 2015-17.
Hayo yamebainika leo katika
kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Naibu
Waziri wa afya Zanzibar Harusi Saidi Suleiman wakati ajibu swalila mwakilishi
wa Chake Chake Suleiman Sarahan Said.
Mwakilishi huyo aliuliza swali Je, suala la uzazi salama kwa akinamama na mtoto ni tatizo kubwa
au kama limepungua kwa asilimia ngapi.
Naibu huyo alilieleza
bara kuwa kwa sasa hali ya Vifo
kwa kina mama imepungua ambapo kwa upande wa watoto wachanga pia vimepungua
kutoka vifo 79 hadi kufikia vifo 56 kati ya vizazi hai laki moja kwa mwaka
2015-17.
Alifahamisha kuwa kwa sasa Wizara yake imeamua kuimarisha
upatikanaji wa huduma muhimu kwa wazazi ili kujinga na tatizo la vifo vya
kina mama na watoto wachanga.
“Serikali inaendelea na azma yake ya kuimarisha miundombinu ya
huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuendelea kutoa elimu ya afya ili
wananchi hususan kina mama wajawazito waweze kujifungua salama” alieleza Naibu
Harusi.
Sambamba na hilo alieleza kuwa Wizara inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za
kiafya ikiwemo kufanya utafi na kutathmini huduma za dharura wakati wa ujauzito,Wakati wa kujifungua na watoto wachanga ili kumuandalia mama mjamzito mazingira
bora ya kujifungua salama.
Akizungumzia sababu zinazochangia vifo vya kina mama na Watoto
wachanga alisema ni pamoja na
uhaba wa elimu ya Afya hususan Maskulini ,imani potofu katika jamii
pamoja na lishe duni kwa mama na mtoto.
“Miundombinu mibovu wa Barabara jambo ni sababu nyengine kubwa
jambo ambalo linawapa wakati mgumu wazazi wakati wakitaka kuvifikia vituo
vya Afya na kushindwa kupata huduma kwa haraka” alieleza Bi Harusi.
No comments:
Post a Comment