NA MWANDISHI WETU,
BAGAMOYO
WAUMINI wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Bagamoyo wametakiwa kufanya kazi ya kushirikiana ili kuweza
kusaidia kazi ya Mungu kusonga mbele na kuwafikia watu wengi.
Wito huo umetolewa na
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Mashariki kati mwa Tanzania, Mchungaji Joseph Mngwabi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya
uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa jipya la kisasa la Waadiventista
wasabato Bagamoyo uliofanyika juzi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
“Mkifanya kazi kwa
kushirikiana na kwa lengo moja, mtafanikiwa sana kufikia malengo mliyojiwekea
na hii itasaidia sana kufanya kazi ya Mungu isonge mbele”alisema Mchungaji
Mngwabi.
Awali katika hotuba ya
kumkaribisha mgeni rasmi Mchungaji wa mtaa wa Bagamoyo Mch.Melkizedeki Wanjala,
alisema kuwa kanisa la Waadventista Wasabato Bagamoyo lilitengwa kuwa Kanisa
kutoka Kanisa mama la Mwenge mnamo mwaka 1995,ambapo hadi kufika mwaka 2001
Kanisa lilifanikiwa kuwa wa jengo lake la kuabudia eneo la Tandika-Bagamoyo.
Lakini kufikia mwaka 2013 idadi kubwa ya waumini iliongezeka, hali hii
ilipelekea jengo la awali kutotosha, hivyo kuwa na hitaji la kuwa na Kanisa kubwa
zaidi.
Akizungumzia ujenzi wa
jengo jipya la Kanisa Mchungaji Wanjara amesema kuwa jengo hilo litagharimu jumla
ya Sh. Milioni 450 hadi kukamilika kwake , hivyo amewataka washiriki
kushirikiana kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi huo huku akinukuu Maandiko
Matakatifu kutoka kitabu cha Kutoka 25:8 yanayosema “nao wanifanyie patakatifu
ili nipate kukaa kati yao.
No comments:
Post a Comment