HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 12, 2019

Benki ya CRDB yafurahia faida mara dufu 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya benki hiyo 2018.
 Baadhi ya maofisa waandamizi wa benki ya CRDB.
 Baadhi ya wakurugenzi wa benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya maofisa waandamizi wa benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Fedha CRDB, Fredrick Nshekanabo, akijibu akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari.
Katibu wa Benki ya CRDB John Rugambwa (kushoto), akiwa na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa, akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini.
 
NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema ofisi yake imetengeneza faida ya Sh. bilioni 64.1 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 77.7 kutoka Sh. bilioni 36.2 iliyopatikana mwaka 2017.

Akizungumza na baadhi ya watendaji wa benki hiyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana kuhusu ufanisi wa CRDB kwa mwaka 2018 na ongezeko la faida, alisema umekuwa mwaka wa mafanikio kwao.

“Licha ya kuwa mwaka wa mabadiliko ya uongozi, mapato na faida ya benki yetu yaliongezeka mara dufu kutokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na yasiyo ya riba… tuliongeza kiwango cha mikopo na kushusha uwiano wa mikopo chechefu.

“Mikopo tuliyopewa na wateja iliongezeka huku tukiongeza amana kwa wateja wapya kupitia huduma za kidijitali ikiwemo simuBanking,” alisisitiza Nsekela.

alisema ni utaratibu wa benki hiyo ya kwanza kwa ukubwa Tanzania kujiwekea mikakati ya miaka mitano ulioanza mwaka 2018 huku akisisitiza kwamba wamejipanga kuyavuka malengo waliyojiwekea.

“Tunaendelea kujiimarisha na kuipitia mara kwa mara mifumo yetu ya utoaji wa huduma kwa wateja wetu ili kuhakikisha tunakidhi mahitaji ya soko,” alisema mkurugenzi huyo mtendaji.

Kwa mujibu wa Nsekela, mapato halisi ya riba katika benki ya CRDB kwa mwaka 2018 yaliongezeka kwa Sh. bilioni 33.1 na kufikia Sh. bilioni 442.8 kutoka Sh. bilioni 409.7 bilioni za mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia nane.

“Tulifanikiwa kupunguza kiwango cha mikopo chechefu kwa asilimia 4.1 na kufikia asilimia 8.5 kutoka asilimia 13.6 iliyokuwepo mwaka 2017 lengo letu ishuke zaidi hadi chini ya asilimia tano.

“CRDB ni benki ya tatu kwa ukubwa Afrika Mashariki na tumeendelea kukua, mali za benki zimeongezeka kwa asilimia 2.3 kutoka Sh. trilioni 5.9 Desemba mwaka 2017 hadi Sh. trilioni sita mwaka 2018.

“...Ni imni yetu kwamba ongezeko hilo ni matokeo ya mpango mkakati la benki kuongeza kiasi cha mikopo inachotoa ili kuimarisha mapato yatokanayo na riba,” alisisitiza Nsekela.

Aliyetaja maeneo muhimu ya ufanisi ya mwaka uliopita kuwa ni ongezeko la amana za wateja kwa asilimia 7.8 hadi Sh. trilioni 4.66 kutoka Sh. trilioni 4.33 na mapato ya riba yaliongezeka kutoka Sh. bilioni 560.3 hadi Sh. bilioni 586.3.

Kuhusu mkakati wa benki kuwakopesha wajasiriamali wadogo na wa kati, Mkurugenzi wa Fedha CRDB, Fredrick Nshekanabo alisema wametenga zaidi ya Sh. bilioni 440 kwa ajili ya mikopo ya wajasiriamali hao.

“Tunaendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuikuza Tanzania ya viwanda kwa kuwa benki yetu inafanyakazi kwa karibu zaidi na serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages