Na Mwandishi Wetu
Dar es
Salaam. Jumla ya klabu 10 zimethibitisha kushindana katika mashindano ya klabu
bingwa ya mchezo wa kuogelea yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la
Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia leo
Jumamosi.
Klabu ambazo
zitashiriki katika mashindano hayo ni i Bluefins, Champion Rise, Mis Piranhas,
klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC), FK Blue na Wahoo ya Zanzibar.
Nyingine
kuwa ni ISM-Moshi, ISM-Arusha,FK Blue Marlins, Talis-IST na mabingwa watetezi,
Dar es Salaam Swim Club (DSC).
Mashindano
hayo ambayo yatamalizika kesho Jumapili, yamedhaminiwa na IST, Azam, Pepsi,
Asas, Samsung, DTB Bank, Kaka’s, Food Lovers na Snow Cream.
Wadhamini wengine
ni Kastipharn Ltd, Ruru Logistics, Knight Support, Oppotune Travel ltd, Pyramid
Consumers, Print Galore, ITV Media, Clouds FM, Subway, NMB Bank and Umoja Grand
Belt na Road Restaurant.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa
waogeleaji wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi wamewasili kwa ajili ya kushiriki
katika mashindano hayo.
Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Maia Tumiotto , Collins
Saliboko, Dennis Mhini, Chichi Zengeni, Natalia Sanford, Smriti Gorkarn na Delvin Barick ambao wote wanasoma shule ya
from St Felix , Uingereza.
Wengine ni Christian Shirima anayetokea nchi ya Ukraine, Isam Sepetu (Afrika Kusini), Hilal Hemed Hilal
na Kangeta wanaotokea klabu ya Hamilton Aquatic ya Dubai.
Alisema kuwa
mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi siku ya Jumamosi na
waogeleaji watashindana katika staili tano ambazo ni Freestyle, Breaststroke,
Butterfly, Backstroke na Individual Medley.
Kwa mujibu
wa Hadija, waogeleaji hao pia watashindana katika relay katika mashindano
ambayo yamepitishwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea Duniani (Fina) kuwa ya
kutafuta alama za kufuzu mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini
Korea mwezi Julai.
“Tunatarajia
kuona ushindania mkali kwa waogeleaji
wetu ili kutafuta nafasi ya kufuzu mashindano ya dunia. Waogeleaji wengi wapo
katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo, bado
tunahitaji wadhamini wa mashindano haya,” alisema Hadija.
Kwa mujibu
wa Hadija, kutakuwa na jumla ya vipengele
vya mashindano 108 na kila klabu imetakiwa kuwakilishwa na waogeleaji
wawili katika kila kipengele cha mashindano ambavyo pia vimepangwa kutokana na
umri.
No comments:
Post a Comment