Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Naiz Majani (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo na washindi wa kwanza wa Km. 21 mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya mbio za Heart Marathoni zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam. Lengo la mbio hizo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo fedha zilizopataikana zitafanya upasuaji kwa watoto 50 kuanzia tarehe 7/5/2019.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Naiz Majani (kulia) akiwa na bibi yake
Magreth Mngofi (kushoto) mara baada ya kumaliza kukimbia mbio za Heart
Marathoni zilizofanyika Aprili 28 jijini Dar es Salaam. Dkt. Naiz alikimbia
umbali wa Km. 10 na Bibi Magreth alikimbia umbali wa Km. 5.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani amechaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Taasisi
kwa mwaka 2019.
Dkt. Naiz amechaguliwa
na Kamati ya kuchagua mfanyakazi bora kwa kuangalia utendaji wake wa kazi katika kutoa huduma ya
matibabu ya moyo kwa watoto, bidii ya kazi , kufanya kazi kwa kujituma na kufanya
kazi kwa uvumilivu. Pia ushirikiano mzuri baina yake na wafanyakazi pamoja na uongozi wa
Taasisi.
Mfanyakazi
huyu bora wa mwaka 2019 atapewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni tatu,
cheti na ngao ya kutambua mchango wa kazi anazozifanya.
Fedha hizo
atakabidhiwa mkoani Mbeya na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mgeni rasmi
katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani
zitakazofanyika tarehe 01/05/2019
Imetolewa na: Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
No comments:
Post a Comment