Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike kulia pamoja
na Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi. Marry Ndalo wakiwa tayari
kwa ufunguzi wa kikao cha Kamati Ndogo ya Ardhi kujadili suala la umiliki wa
ardhi kwa wanawake mapema leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Idara ya Jinsia wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Julius
Mbilinyi kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Bi.
Marry Ndalo wakiwa tayari kwa ufunguzi wa kikao cha Kamati Ndogo ya Ardhi
kujadili suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake mapema leo Jijini Dodoma.
Na
Anthony Ishengoma
Kamati ya Uwezeshaji
Wanawake katika Umiliki na Matumizi ya Ardhi inakaa leo Jijini Dodoma
kujadili na kuhainisha fursa na vikwazo
vya kuwezesha umiliki wa ardhi kwa wanawake na kupanga mikakati ya
kufikia lengo la wanawake kumiliki na kutumia ardhi kwa maendeleo yao.
Akifungua Kikao cha Kamati
hiyo mapema leo Jijini Diodoma Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa
kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kinajaadili namna bora ya kuwawezesha wanawake
kumiliki na kutumia ardhi katika
kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha Bw. Golwike ameongeza
kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria na jitihada mbalimbali kutoka kwa wadau wa kusaidia
wanawake kunufaika na ardhi bado kuna vikwazo vinavyoathiri wanawake kumiliki
ardhi kwa sababu mbalimbali zikiwemo mila na desturi, ufahamu mdogo wa umiliki
ardhi ikiwemo ukosefu wa dhamana za kiuchumi.
Bw. Golwike amewataka
wajumbe wa kamati hiyo kupitia kwa Taasisi wanazotoka kuwa wabunifu wakwenda na
ubunifu wa sayansi na teknolojia katika kuwawezesha wanawake kumiliki na
kutumia ardhi kama njia ya kujikwamua kiuchumi.
Akitoa ufafanuzi kwa
vyombo vya habari vilivyotaka kujua hasa lengo la Kamati hiyo ndogo ya Ardhi
Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii
Bw. Julius Mbilinyi amesema kuwa Kamati hii iliundwa ili kufikia Malengo
Endelevu na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kwa kuhakikisha
wanawake wanapata fursa ya kumiliki ardhi na kuitumia kujiletea maendeleo.
Aidha Bw. Mbilinyi
ameongeza kuwa kamati ndogo ya ardhi imejiwekea mikakati ya kuhakikisha
wanawake wanaondokana na vikwazo vya muda mrefu kama vile mila na
desturi ili waweze kutumia fursa ya kumiliki ardhi na kuitumia kujiendeleza
kiuchumi na kuwa Sehemu ya uchumi mpana wa Nchi yetu.
‘’Suala kubwa sio
umiliki wa ardhi kwa wanawake lakini pia ni kuangalia namna bora wanawake hawa
wanaitumia fursa ya mali hisa ya ardhi kujiletea maendeleo ili wawe sehemu ya
uchumi mpana wa Taifa letu”. Aliongeza Bw. Mbilinyi.
Wakati huohuo
Bi.Marry Ndalo kutoka Shirika la Kimataifa la Care ameongeza kuwa Kamati hiyo
kimsingi inawakutanisha wadau kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kuwaweka
pamoja kujadiliana masuala ya ardhi lakini pia kupata taarifa kuhusu idadi ya
Wanawake wanaomiliki ardhi na wasio miliki ardhi ili kuweka wanawake katika
mjadala wa ardhi ambao inaajiri wanawake wengi.
No comments:
Post a Comment