NA JOHN MARWA
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz
anayetamba na kibao chake cha ‘You Are The Best’ amewapigisha pamba mashabiki
zake katika duka la GSM Mall Pugu ukiwa
ni muendelezo wa kutoa zawadi kwa mashabiki zake.
Washindi wawili mmoja wa kiume Charles Allen na
wakike Sarahati Rashid wameibuka washindi kwa mujibu wa Dimpoz baada ya kupitia
posti za mashabiki zake wanatumia muda wao mwingi kuposti kazi zake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika duka
la GSM Mall ambalo aliwafanyia shoping, Nyota huyo kutoka Rock Star alisema alifurahishwa
na jinsi Charles na Sarhati walivyotoa mchango mkubwa kusapoti kazi zake.
“Nimeangalia ni shabiki yupi anamchango mkubwa wa
kusapoti kazi zangu nikagundua kuwa Charles na Sarhati wamekuwa wanajitoa sana
kusapoti kazi zangu, japo wapo wengi wanaofanya kama wao.
“Nimewachagua mwenyewe kuwawakilisha mashabiki zangu
wengine kwa hiki kidogo lakini chenye hadhi, kwa kushirikiana na GSM Mall nimeamua
kuwafanyia shoping kwa kuzingatia jenda japo sio mara ya kwanza na ya mwisho
nadhani nimeanza na hawa kama nyimbo yangu inavyosema you are my best.
“Ni kweli sijawahi kufanya kitu kama hiki lakini ni
vizuri vile tunavyovipata tugawane na marafiki na mashabiki si kitu kibaya
wanapenda, yawezekana siku Mungu akijalia tukipata kikubwa zaidi kuna siku
labda ntatoa gari yote kheri,”alisema
No comments:
Post a Comment