HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 07, 2019

Ivo ahimiza timu kujitosa fainali ‘Castle Lager Africa 5s

NA MWANDISHI WETU

BALOZI wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda amewaomba wamiliki wa Baa kuunda timu bora za kiushindani zitakazoshiriki fainali ya Bonanza la timu 32 kutoka jijini Dar es Salaam.

Mnyumkano wa timu hizo, ni kupata timu moja bora zaidi ambayo itaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu hapa nchini.

Mapunda aliyasema hayo jana kwa Waandishi wa habari wakati akijiandaa rasmi na ziara ya kutembelea Baa 60 za jijini Dar es Salaam zilizoingia kwenye mchakato wa kiushindani kupitia promosheni zinazoendelea kwenye Baa hizo.

Akiwa katika ziara hiyo, Mapunda amewaomba wamiliki hao wajitahidi kuunda timu bora kwani wanatarajia kuwa na ushindani mkubwa ambao mwisho wa siku utawapatia timu moja kutoka Baa moja na kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Africa.

“Mashindano haya yanafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza lakini ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia nhini(TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager,” alisema Ivo.

Ivo amesema, ingawa ni mara ya kwanza kwa Tanzania, yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika hivyo kitendo cha fainali hizo za Afrika kufanyika nchini, ni fursa kwa Tanzania.

“Fainali za Africa zinafanyika hapa Tanzania, nawasihi wamiliki wa Baa shiriki, tutambue Bingwa wa fainali ya Bonanza atawakilisha Watanzania wote,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa maana hiyo uundaji wa timu zetu na maandalizi kwa ujumla yanapaswa kuwa mazuri,” alisema Ivo, Balozi wa Castle Lager Tanzania.

Ivo alisema mwaka jana Tanzania ilishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, yaliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia.

“Binafsi niwapongeza sana Wadhamini wa mashindano haya Castle Lager kwa kudhamini mashindano haya ambayo yanawapa fursa wanywaji wao kushiriki michezo.

“Mwisho wa siku unatupa nafasi ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania. Lakini pia niwashukuru kwa kuniona mimi kama nastahili kuwa Balozi wa Castle Lager Africa 5s kwa hapa nchini Tanzania.

“Nafahamu Mchakato wa kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zinazoendelea katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam” alisema Ivo.

Kuhusu kuingia kuingia hatua ya 32 bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha maalumu katika baa husika kwa ajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua bia ya Castle Lager.

“Niwaombe watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto zao” alisema Ivo na kuongeza kuwa wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra kutokea.

No comments:

Post a Comment

Pages