NA JOHN MARWA
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameiomba kamati ya hamasa kwa timu ya
taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kugeukia upande wa timu ya taifa chini ya miaka
17 (Serengeti Boys).
Serengeti Boys ambao ni wenyeji wa fainali za
mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo ambazo zitafanyika kwa mara ya
kwanza hapa nchini kuanzia Aprili 14 hadi 28 mwaka huu.
Karia ameiomba kamati hiyo iliyoko chini ya
mwenyekiti wake Paul Makonda, kuhamishia hamasa kwa Serengeti Boys ili waweze
kuweka historia nyingine kwenye soka la Tanzania kwa kubakiza taji hilo ama
kupata naafasi ya kufuzu fainali za Dunia nchini Brazili.
"Namuomba mheshimiwa Makonda alibebe hili
nalo ili kama nchi tuweze kuipeperusha vema bendera ya Tanzania, naamini
inawezekana kwa maslahi mapana ya taifa.
"Lengo letu ni kutwaa uchampion kwa faida
ya kuwa wenyeji lakini kama itashindikana japo hilo la kushindwa halipo
kichwani mwetu basi tupate nafasi ya kwenda kombe la dunia," alisema Karia
na kuongeza kuwa.
"Ni wazi muda ni mchache uliosalia lakini hakuna budi kushikana mikono na
kulibeba tukio zito lililopo mbele yetu."
No comments:
Post a Comment