NA JOHN MARWA
SHIRIKISHO la Soka
Tanzania TFF kupitia Rais wake Wallece Karia, amesema ukiukwaji wa haki za kurusha
matangazo kwa michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Azam FA, linachangia kuikosesha
Serikali mapato.
Hatua hiyo imekuja mara
baada ya hivi karibuni kuibuka Luninga zenye Cable ambazo zinakiuka utaratibu
huo jambo ambalo linaingilia haki za
mwenye mkataba wa kisheria kutoa huduma hiyo.
Karia amewataka wanaohusika
na michezo hiyo kuacha mara moja kwani aliyepewa haki ya kurusha matangazo hayo ni Azam Tv na
amekuwa akilipa kodi kwa wakati kama ambavyo walivyokubaliana kwenye mkataba
wao.
Amesema hali hiyo
inasababisha ligi hiyo kukusa udhamini Mkuu
hivyo wameona watoe onyo hilo kwa wote wanaofanya vitendo hivyo kuacha
mara moja kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria kumlinda mdhamini mzawa
aliyejitokeza kudhamini ligi hiyo.
“Siku za hivi karibuni
kumejitokeza wimbi kubwa la Luninga za Cable ambazo zinaiba matangazo kutoka
Azam na wanaonesha bila kufanya makubaliano na aliyepewa haki au TFF jambo
ambalo linaweza kusababisha Azam ambao ni wadhamini kujitoa kwa kukosa mvuto.
“TFF hatuna mkataba wowote na Luninga za Cable
kuendelea kufanya hivyo wanakiuka kanunini na sheria zilizowekwa hivyo tunatarajia kwenda Mahakamani kufungua
kesi wanaohusika kufanya jambo hili wakamatwe wafikishwe kwenye vyombo vya dola,
” amesema Karia na
kuongeza kuwa.
“Ukiukwaji huo hadi sasa
umesababisha athari kubwa ikiwemo
serikali kupoteza mapato na Azam kama mdhamini aliyeuziwa haki ya matangazo
hayo kudhoofisha uchumi wake,”.
Alisema ili kuhakikisha
wanadhibiti jambo hili ambalo linachangia kurudisha nyuma watu wenye uwezo
kuwekeza kwenye mchezo wa soka, wameunda kamati kutoka TFF, Azam Media na Jeshi
la Polisi kwa ajili ya kuwakamata wote ambao wanafanya hivyo kuwapeleka kwenye
vyombo vya dola.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Azam Tv Tido Muhando alisema hata kwa watu wanaorusha matangazo
hayo kwa njia ya You tube ni kinyume na
makubaliano na kwamba hiyo ni biashara kama biashara zingine hivyo lazima
utaratibu uheshimiwe kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
“Nawapongeza TFF,kwa
kuliona hilo jambo ambalo limekuwa likituumiza kichwa kwa kiasi kikubwa na
kuwaomba wanaofanya hivyo waache mara moja na kuheshimu taratibu na kanuni
zilizowekwa” amesema Tido.
No comments:
Post a Comment